Nenda kwa yaliyomo

Moabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moabu inaonyeshwa katika rangi ya zambarau katika ramani hii kuhusu hali ya mwaka 830 KK.
Jiwe la Mesha lilivyopigwa picha mwaka 1891 hivi.

Moabu (kwa Kiebrania מוֹאָב Mo'av au Môʼāḇ, "Mbegu ya baba"; kwa Kigiriki Μωάβ Mōav; kwa Kiarabu مؤاب) ni jina la kihistoria la eneo la milimani upande wa mashariki wa Bahari ya Chumvi ndani ya nchi ya kisasa ya Yordani. Ilikuwako kati ya Edomu upande wa kusini na Amoni upande wa kaskazini.

Zamani eneo hilo lilikuwa ufalme wa Wamoabu. Mji wake mkuu uliitwa Diboni na maghofu yake yapo karibu na mji wa Dhiban wa kisasa.

Kati ya shuhuda za kiakiolojia za kabila hilo, muhimu zaidi ni Jiwe la Mesha, linaloeleza ushindi wao dhidi ya mwana wa mfalme Omri wa Israeli.

Sawa na Isreli Moabu ilikuja chini ya mamlaka kwanza ya Ashuru na baadaye ya milki ya Babeli. Mwaka 582 KK mfalme Nebukadnezzar II wa Babeli alifanya Moabu kuwa sehemu ya milki yake; hivyo ilikuwa sehemu ya ufalme wa Uajemi baadaye. Wakati wa utawala wa Kiajemi Moabu ilipotea kama taifa la pekee. Makabila ya Waarabu walianza kuingia na kukalia sehemu kubwa za nchi na wakazi waliacha lugha yao wakatumia Kiaramu badala ya lugha yao ya awali.

Uhusiano kati ya Moabu na Israeli ya Kale[hariri | hariri chanzo]

Katika masimulizi ya Biblia "Moabu" ilikuwa awali jina la mwana wa Lutu na Wamoabu walikuwa ukoo wake. Kufuatana na kitabu cha Mwanzo 19:30-38 walikuwa na asili moja na Wanaisraeli maana Moabu anatajwa kama mjukuu wa Abrahamu kupitia Lutu aliyemzaa Moabu na binti yake mkubwa.

Kulingana na habari za Biblia uhusiano kati ya Moabu na Israeli ya Kale mara nyingi haikuwa nzuri wakapigana mara nyingi kivita. Lakini walikuwa karibu katika habari nyingi za jamii na utamaduni wao; lugha yao ilifanana sana na Kiebrania jinsi inavyonoekana kwenye matangazo ya jiwe la Mesha.

Pamoja na masimulizi yanayoonyesha uhusiano mbaya kama habari za Bileamu (Hesabu 22-24) au za Egloni na Ehudi (Waamuzi 3, 12 ff) kuna pia habari za kinyume. Kitabu cha Ruthu inasimulia habari za mwanamke wa Moabu anayeonyeshwa lama kielelezo na anaendelea kuingia kati ya mababu wa mfalme Daudi.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Routledge, Bruce. 'Moab in the Iron Age:Hegemony, Polity, Archaeology,' 2004. The most comprehensive treatment of Moab to date.
  • Bienkowski, Piotr (ed.) Early Edom and Moab: The Beginning of the Iron Age in Southern Jordan (1992).
  • Dearman, Andrew (ed.) Studies in the Mesha inscription and Moab (1989).
  • Jacobs, Joseph and Louis H. Gray. "Moab." Jewish Encyclopedia. Funk and Wagnalls, 1901–1906, which cites to the following bibliography:
  • Tristram, The Land of Moab, London, 1874;
  • George Adam Smith, Historical Geography of the Holy Land, ib. 1897;
  • Clermont-Ganneau, Recueil d'Archéologie Orientale, ii. 185-234, Paris, 1889;
  • Baethgen, Beiträge zur Semitischen Religionsgeschichte, Berlin, 1888;
  • Smith, Rel. of Sem. Edinburgh, 1894. J. L. H. G.
  • Hertz, J.H., The Pentateuch and Haftoras: Deuteronomy, Oxford, 1936, Oxford University Press.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]