Mnuvi (Triglidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mnuvi
Mnuvi kusi (Chelidonichthys capensis)
Mnuvi kusi (Chelidonichthys capensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Scorpaeniformes (Samaki kama mabocho)
Nusuoda: Scorpaenoidei (Mabocho)
Familia: Triglidae
Risso, 1826
Ngazi za chini

Jenasi 9 na spishi 126, 22 katika Afrika:

Minuvi au panzi-bahari ni samaki wa baharini wa familia Triglidae katika oda Scorpaeniformes ambao wana mapeziubavu makubwa yanayowasaidia kuruka juu ya maji, lakini huumbia umbali mfupi kuliko panzi-bahari wengine wa familia Exocoetidae. Wanafanana na minuvi wa nusuoda Platycephaloidei.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Hawa ni samaki wa sakafu ya bahari wanaoishi mpaka kina cha mita 200, ingawa wanaweza kupatikana katika maji kame. Spishi nyingi zina urefu wa sm 30 hadi 40. Wana fuvu gumu lisilo la kawaida na spishi nyingi pia zina magamba ya deraya kwenye mwili wao. Sifa bainifu nyingine ni uwepo wa "msuli wa kupiga ngoma" ambao unafanya sauti kwa kukipiga kibofuhewa. Wakikamatwa hufanya sauti ya kuguna kama chura, ambayo ni asili ya jina la tanakali "gurnard" kwa Kiingereza. [

Minuvi wana "miguu" sita kama miiba, mitatu kwa kila upande. Miguu hiyo kwa kweli ni tindi kinamo ambazo mara moja zilikuwa sehemu za mapeziubavu. Wakati wa maendeleo tindi hizi zinajitenga kutoka sehemu nyingine ya pezi na kuendelea kuwa "miguu ya mbele" iliyo kama ndevu za mdudu. Tindi hizi zinaweza kutumika kutembea kwenye sakafu ya bahari na pia kuchunguza mchanga ili kutafuta chakula, kwa sababu zinaweza kudaka kemikali na kuwa nyeti sana kwa asidi amino zilizoenea katika invertebrata wa bahari.

Uvuvi na chakula[hariri | hariri chanzo]

Minuvi wana nyama nyeupe imara ambayo hushiriki pamoja vizuri wakati wa kupika na kuifanya vizuri katika supu na michuzi. Hukamatwa na kuuzwa sana huko pwani ya Afrika ya Mashariki. Katika maji ya Uingereza mara nyingi walikamatwa bila kusudi na kukataliwa. Hata hivyo, kama spishi nyingine ilipungua chini na kuwa na bei kubwa zaidi, kutoka mwaka 2014 minuvi walikuwa maarufu zaidi nchini Uingereza. Minuvi huonekana sasa pia katika masoko ya samaki huko Marekani, huku wameuzwa nchini kwa Bara la Ulaya tangu miaka mingi. Vyanzo fulani vinasema kwamba minuvi wana mifupa mingi na hawana ladha, na kwa kawaida kuuzwa kwa bei nafuu kiasi; wengine wanasifu ladha na usisisi wao. Nyama ya samaki hawa hutumiwa kwa kawaida katika mlo wa Kifaransa bouillabaisse.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mnuvi (Triglidae) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.