Nenda kwa yaliyomo

Mtunguja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mndulele)
Mtunguja
(Solanum spp.)
Mtunguja wenye tunguja bichi
Mtunguja wenye tunguja bichi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Solanales (Mimea kama mnavu)
Familia: Solanaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mnavu)
Jenasi: Solanum
L.
Spishi: S. incanum L.

S. schumannianum Dammer
S. zanzibarense Vatke

Mtunguja, mtunguja-mwitu, mtura, mtula, mtulwa, mtua, mtuatua, mndulele, mnyanya-mwitu au mnyanya-pori ni majina mbalimbali ya mimea ya familia Solanaceae. Fasihi andishi (ya kisayansi na ya umma) haidhihirishi majina gani hutumika kwa spishi gani. Inaonekana kwamba majina yote hutumika kwa Solanum incanum (kwa Kiingereza thorn apple) lakini majina kadhaa hutumika kwa spishi nyingine pia, hasa Solanum schumannianum na Solanum zanzibarense.

Mitunguja ina sumu lakini kuna namna ambazo majani na matunda yake huliwa baada ya kupikwa. Yote hutumika kama mitishamba, k.m. dhidi ya magonjwa ya ngozi, ya koo, ya meno na ya tumbo na dhidi ya maumo ya nyoka.

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtunguja kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.