Nenda kwa yaliyomo

Mlangobahari wa Tsugaru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

41°29′57″N 140°36′57″E / 41.49917°N 140.61583°E / 41.49917; 140.61583

Rasi ya Tsugaru na Mlangobahari wa Tsugaru
Tappi Misaki

Mlangobahari wa Tsugaru (kwa Kiingereza: Tsugaru Strait, kwa Kijapani: 津軽海峡 Tsugaru Kaikyō) ni sehemu nyembamba ya bahari iliyopo kati ya visiwa vya Honshu na Hokkaido nchini Japani. Iko katika kaskazini ya Japani. Inaunganisha Bahari ya Japani na Pasifiki[1]. Jina lake linatokana na Tsugaro ambayo ni sehemu jirani ya Mkoa wa Aomori kwenye kisiwa cha Honshu.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kina kirefu cha maji ni mita 490. Mkondo wa maji vuguvugu unapita humo kutoka kusini kuelekea kaskazini unaoitwa kwa Kijapani Tsushima-kairyū.[2]

Chini ya mlangobahari kuna njia ya reli inayopita ndani ya handaki chini ya bahari. Reli hii ilichukua nafasi ya feri iliyowahi kubeba watu na mizigo kutoka kisiwa kimoja kwenda kingine kwa masaa manne.

  1. Nussbaum, Louis-Frédéric. (2005). "Tsugaru Kaikyō" in Japan Encyclopedia, p. 998.
  2. Nussbaum, "Tsushima Kaikyō" at p. 1003.
Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlangobahari wa Tsugaru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.