Mkweme
Mandhari
Mkweme (Telfairia spp.) | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mkweme mashariki
(Telfairia pedata) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 3:
|
Mikweme ni mimea ya jenasi Telfairia katika familia Cucurbitaceae. Ina umbo la kamba na kutambaa juu ya miti yenye shina kubwa. Matawi yake yanafikia urefu wa mita 30.
Matunda yake ni makubwa sana; yale ya mkweme mashariki yanaweza kufikia kg 15. Mbegu huitwa kweme na hutumika kama chakula na kwa kutengeneza mafuta. 25% ni protini na 55% ni mafuta, hivyo zinafaa sana kama chakula bora, kwa mfano kwa akina mama baada ya kujifungua.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Telfairia batesii, Mkweme-mwitu (Bush oysternut)
- Telfairia occidentalis, Mkweme Magharibi (Fluted pumpkin)
- Telfairia pedata, Mkweme Mashariki (Oysternut)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mkweme magharibi
-
Makweme mashariki
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkweme kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |