Mkindo, Hembeti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkindo ni kijiji cha Tanzania kipo katika kata ya Hembeti, wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro. Kijiji hiki kina jumla ya shule za msingi mbili. Shule ya msingi mkindo A na Shule ya msingi mkindo B. Pia kijiji kina zahanati moja na pia inagulio (soko la wiki) ambalo hufanyika kila jumamosi.

Lakini kwa sasa kijiji cha MKINDO ni kata mpya baada ya kata ya HEMBETI kuzalisha kata hiyo mpya. Kijiji cha MKINDO nacho pia kikagawanyika na kuzalisha vijiji vya MKINDO na BUNGOMA. Hivyo kata ya Mkindo ina vijiji vinne ambavyo ni Mkindo,Kambala,Mndela na Bungoma.

Shughuli kubwa ya wakaazi wake ni kilimo na zao kuu ni mpunga na mahindi.

Kuna bonde kubwa la mpunga ambalo ni maarufu sana linaitwa Mgongola. Pia wananchi wanajishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika katika shamba linaloitwa SIDU.