Nenda kwa yaliyomo

Akili ya binadamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mind)
Ramani ya ubongo[1] ikionyesha sehemu zake zinavyohusika na kazi tofautitofauti.
Mchoro wa René Descartes[2].

Akili ya binadamu (kwa Kiingereza "mind"[3]) ni kipawa kinachowezesha kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo. Ni ufahamu unaotumia ubongo na unaomwezesha binadamu hata kutofautisha jambo kwa wema na ubaya wake upande wa maadili na hatimaye kumuongoza katika kufanya maamuzi kwa kutumia hiari yake[4].

Dhana kuhusu asili ya akili ya binadamu zinatofautiana, vilevile na maelezo mengine mengi, kulingana na dini, falsafa na sayansi[5] husika.

Jambo mojawapo la msingi ni kuelewa kama akili hiyo ya pekee inategemea tu ubongo uliokua sana katika binadamu kuliko katika spishi nyingine au kuna athari kubwa ya roho ndani yake. Hii ni kwa sababu walichoweza kufanya watu hakifanani kabisa na wanyama walichofanya, hata wale walio na ujirani naye kibiolojia kama sokwe.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Oliver Elbs, Neuro-Esthetics: Mapological foundations and applications (Map 2003), (Munich 2005)
  2. Descartes, R. (1641) Meditations on First Philosophy, in The Philosophical Writings of René Descartes, trans. by J. Cottingham, R. Stoothoff and D. Murdoch, Cambridge: Cambridge University Press, 1984, vol. 2, pp. 1–62.
  3. "mind – definition of mind in English | Oxford Dictionaries". Oxford Dictionaries | English. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-19. Iliwekwa mnamo 2017-05-08. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  4. Başar, Erol (2010). Brain body mind oscillations in scope of uncertainty principle. New York: Springer. uk. 5. ISBN 978-1441961365.
  5. Harnad, S.R., Steklis, H.D., & Lancaster, J.E. (1976). "Origins and evolution of language and speech". Annals of the New York Academy of Sciences. 280 (1): 1–2. Bibcode:1976NYASA.280....1H. doi:10.1111/j.1749-6632.1976.tb25462.x.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akili ya binadamu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.