Mick Jagger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mick Jagger (2003)

Michael Philip "Mick" Jagger (amezaliwa 26 Julai 1943) ni mwanamuziki wa Uingereza, mtayarishaji na mwigizaji. Anajulikana zaidi kwa kuwa mwimbaji wa bendi ya The Rolling Stones.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Jagger anajulikana kwa mahusiano yake mengi. Alimwoa Bianca De Macias, mzaliwa wa Nikaragua, tarehe 12 Mei 1971. Ilikuwa ndoa ya Kikatoliki huko Saint-Tropez, Ufaransa. Mwishoni mwa 1977, alianza uhusiano na mwanamitindo Jerry Hall [1] wakati bado alikuwa katika ndoa na Bianca. Jagger na Hall waliishi pamoja kwa miaka mingi. Walifunga ndoa tarehe 21 Novemba 1990, katika sherehe ya Kihindu nchini Indonesia. Ndoa hiyo ilikwisha mnamo Agosti 1999.

Alikuwa kwenye uhusiano na L'Wren Scott (1964-2014) kutoka mwaka 2001 hadi alipojiua mnamo 2014.

Mnamo Machi 2019, Jagger alilazimika kuahirisha ziara yake kwa sababu za kiafya. Siku chache baadaye ilitangazwa kwamba angefanyiwa upasuaji wa kubadilisha valvu ya moyo. [2]

Jagger ana watoto saba kwa wanawake wanne: [3]

 • Na Marsha Hunt, ana binti Karis Jagger Hunt (aliyezaliwa 4 Novemba 1970)
 • Na Bianca Jagger, ana binti Jade Sheena Jezebel Jagger (aliyezaliwa 21 Oktoba 1971). [3] [4]
 • Na Jerry Hall ana binti Elizabeth Scarlett Jagger (aliyezaliwa 2 Machi 1984), mtoto wa kiume James Leroy Augustin Jagger (amezaliwa 28 Agosti 1985), binti Georgia May Ayeesha Jagger (aliyezaliwa 12 Januari 1992) na mtoto wa kiume Gabriel Luke Beauregard Jagger (amezaliwa 9 Desemba 1997 ) [3]
 • Na Luciana Gimenez, ana mtoto wa kiume Lucas Maurice Morad Jagger (aliyezaliwa 18 Mei 1999). [3]

Utajiri[hariri | hariri chanzo]

Utajiri wake ulikadiriwa kuwa dolar za Marekani milioni 190 mnamo mwaka 2010.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Maelezo ya albamu Chati za Uingereza[5] Chati za Marekani Uthibitisho wa idadi iliyouzwa Uingereza / Marekani
1985 She's the Boss 6 (wiki 11 ) 13 (wiki 29 ) UK: Silver

US: Platinum

1987 Primitive Cool
 • Ilitolewa: 14 September 1987
 • Lebo: CBS Records
26 (wiki 5 ) 41 (wiki 20 )
1993 Wandering Spirit 12 (wiki 7 ) 11 (wiki 16 ) US: Gold
2001 Goddess in the Doorway 44 (wiki 10 ) 39 (wiki 8 ) UK: Silver
2007 The Very Best of Mick Jagger 57 (wiki 2 ) 77 (wiki 2 )
2011 SuperHeavy 13 (wiki 5 ) 26 (wiki 5 )

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Fonseca (18 May 2001). Limited Engagement. Entertainment Weekly. Iliwekwa mnamo 5 May 2011.
 2. Nedelman. Mick Jagger's having his heart valve replaced. The technology is better than ever. CNN. CNN. Iliwekwa mnamo 3 April 2019.
 3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Richard Simpson. "Mick has more children to see than Santa." The Daily Mail, 20 December 2004. Retrieved 6 January 2009.
 4. Christopher Andersen "Mick Jagger"
 5. Roberts, David (2006). British Hit Singles & Albums, 19th, London: Guinness World Records Limited, 277. ISBN 1-904994-10-5.