Nenda kwa yaliyomo

Taya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mfupa wa taya)
Taya la chini la binadamu.

Taya (pia utaya; kwa Kiingereza: jaw) ni sehemu ya muundo wa kinywa cha wanyama wengi. Kazi yake ni kushika na kuhamisha chakula mara nyingi pamoja na kukikatakata.

Mataya ya vertebrata

[hariri | hariri chanzo]

Kwenye vertebrata (au wanyama wenye uti wa mgongo) mataya yanajengwa kwa mfupa au gegedu na kupatikana kwa jozi, yaani taya la chini na taya la juu. Kwa spishi nyingi huwa na meno.

Kwenye wanyama wenye miguu minne mifupa ya taya la juu imeunganishwa na mifupa ya fuvu ya ubongo. Taya la chini linaunganishwa kwa njia mbalimbali na taya la juu. Nyoka zinaweza kuachana mataya yote mawili kabisa na hivyo kumeza hata windo kubwa sana.

Kwenye mamalia taya la chini hushikwa kwa kiungo imara na taya la juu na mfumo huu unaweka mipaka kwa uwezo wa kufungua kinywa.

Mataya ya arithropodi

[hariri | hariri chanzo]
Mataya ya kando ya sisimizi.

Kwenye arithropodi kama wadudu mataya yako kando ya kinywa na yamejengwa kwa chitini. Yanashika chakula, pia wanyama wadogo wengine wanaowindwa na kukipasua.

Shida za taya

[hariri | hariri chanzo]

Shida zinazokumba taya ni kama jaw pain ambapo unapatwa na maumivu kwa mataya. Hili laweza kuwa limesababishwa na: ajali uliyopata na taya zako zikaumizwa, sinuses au mshtuko wa moyo (heart attack). Pia misuli inayoshikilia taya yaweza kuwa imeumia.

Kuna watu pia huzaliwa na taya zisizo laini. Endapo unapatwa na shida za taya kama vile kutokuwa laini basi waweza kumuuliza daktari wa meno akuwekee vifaa vya chuma vinavyofungamishwa na kushikisha meno ili mtu aweze kuuma vitu au hata taya zake zinyooke (kwa Kiingereza: dental braces).

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Taya kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.