Nenda kwa yaliyomo

Mbawakimia kahawia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbawakimia kahawia
Micromus africanus
Micromus africanus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Neuroptera (Wadudu walio na mabawa wenye vena nyingi kama kimia)
Nusuoda: Hemerobiiformia (Mbawakimia)
Familia ya juu: Hemerobioidea (Mbawakimia kijani)
Familia: Hemerobiidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 10:

Mbawakimia kahawia ni wadudu wadogo wa familia Hemerobiidae katika oda Neuroptera (wadudu mabawa-vena) walio na mabawa yanayofanana na kimia. Kama jina lao linavyoonyesha wana rangi ya kahawia kwa kawaida, huku mbawakimia kijani (familia Chrysopidae) wakiwa kijani kwa wazi.

Drepanepteryx phalaenoides anayofanana na jani kavu

Mbawakimia kahawia ni wadudu dhaifu wenye urefu wa mwili wa mm 4 hadi 10 na upana wa mabawa wa mm 4 hadi 18, wakubwa zaidi wakiwa spishi za kitropiki. Kwa kawaida mwili wao huwa hudhurungi hadi kahawia, lakini spishi kadhaa ni njano au kijani. Machomzolenzi yana rangi ya kahawia kinyume na mbawakimia kijani walio macho ya rangi ya dhahabu. Mabawa ni mangavu yenye nywele. Mabawa ya spishi fulani, kama zile za jenasi Drepanepteryx, yanafanana na majani makavu.

Vinginevyo, tabia, chakula na mzunguko wa maisha zao ni sawa na mbawakimia kijani.

Matumizi katika udhibiti wa kibiolojia wa wasumbufu

[hariri | hariri chanzo]

Kama vile mbawakimia kijani, wale wa kahawia wanaweza kutumika katika udhibiti wa kibiolojia. K.m., Micromus tasmaniae hukuzwa nchini Australia na Nyuzilandi kwa ajili ya kuuzwa kama wadhibiti wa kibiolojia dhidi ya vidukari.[1].

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Hemerobius nairobicus
  • Hemerobius reconditus
  • Micromus africanus
  • Micromus oblongus
  • Micromus sjoestedti
  • Micromus timidus