Mbamba Bay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mbamba Bay
Barabara kuu wa Mbamba Bay mwaka 2012 (picha ya Tamimo Boehm)
Barabara kuu wa Mbamba Bay mwaka 2012 (picha ya Tamimo Boehm)
Mbamba Bay is located in Tanzania
Mbamba Bay
Mbamba Bay
Viwianishi: 11°17′10″S 34°48′5″E / 11.28611°S 34.80139°E / -11.28611; 34.80139
Nchi Tanzania
Mkoa Ruvuma
Wilaya Nyasa
Idadi ya wakazi
 - 10,066

Mbamba Bay ni jina la makao makuu ya Wilaya ya Nyasa katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kata ya Mbamba Bay ilikuwa na wakazi wapatao 10,066 waishio humo. [1]

Mbamba Bay ufukoni mwa Ziwa Nyasa (picha ya Tamimo Boehm)

Mji wa Mbamba Bay uko kwenye ufuko wa Ziwa Nyasa takriban 20 km upande wa kaskazini wa mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji. Kuna bandari inayohudumiwa na meli SV Songea. Kwa ratiba isiyofuatwa mara wka mara kuna mawasiliano pia na Nkhata Bay huko Malawi ng'ambo ya ziwa halafu kwa mabandari kwenye mwambao wa Kitanzania za Ziwa Nyasa hadi Itungi Port.

Kulikuwa na majadiliano ya kujenga reli Mbamba Bay - Mtwara kwa ajili ya usafiri mfupi kati ya Malawi na Bahari Hindi na pia kwa kuboresha maendeleo katika kusini ya Tanzania (Mtwara Development Corridor).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Nyasa - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chiwanda | Kihagara | Kilosa | Kingerikiti | Liparamba | Lipingo | Lituhi | Liuli | Liwundi | Luhangarasi | Mbaha | Mbambabay | Mtipwili | Ngumbo | Tingi


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mbamba Bay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.