Masimo wa Napoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Masimo.

Masimo wa Napoli (alifariki 361 hivi) alikuwa askofu wa 10 wa mji huo kuanzia mwaka 350 hadi 357, alipopelekwa uhamishoni kwa sababu ya juhudi zake za kutetea imani sahihi dhidi ya Waario[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, pengine mfiadini pia, kwa kuwa kifo kiliwahi kumpata kutokana na mateso yaliyotokana na dhuluma ya kaisari Konstansi II[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Juni[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.