Mary Leakey

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mary Leaky

Mary Douglas Nicol Leakey (*6 Februari 1913 London - 9 Desemba 1996 Nairobi) alikuwa mtaalamu wa akiolojia aliyekuwa maarufu kutokana na kukuta ushuhuda juu ya maendeleo ya watu wa kwanza.

Alikuta na kutambua fuvu fosili ya kwanza ya sokwe mkubwa kwenye kisiwa cha Rusinga na baadaye pia aina ya sokwe iliyofanana zaidi na binadamu inayoitwa Zinjanthropus kwenye bonde la Olduvai. Alikuta pia nyayo za Laitoli zilizo kati ya ushuhuda wa kale kabisa wa watu waliotembea kwa kutumia miguu pekee.

Tangu 1960 alikuwa mkurugenzi wa uchimbaji kwa Olduvai. Baada ya kifo cha mumewe Louis aliendelea kuwa kati ya wataalamu wakuu kwenye uwanja wa paleoanthropolojia akamfundisha pia mwanawe Richard Leaky katika fani hii.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]