Marko na Marseliani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wat. Marko na Marseliani (kulia) pamoja na Mt. Sebastiano. Mchoro wa karne XIV, Paris, Bibliothèque nationale de France.

Marko na Marseliani (walifariki Roma, Italia, 304 hivi) walikuwa Wakristo waliouawa kutokana na imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian wa Dola la Roma[1].

Inasemekana walikuwa ndugu pacha mashemasi; kwa vyovyote walipata kuwa ndugu kwa kufia dini pamoja.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini, pengine pamoja na Trankwilini, Marsya, Nikostrato, Zoe, Kastulo na Tibursi.

Sikukuu yao ni tarehe 18 Juni[2] au 18 Desemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.