Nenda kwa yaliyomo

Marissa Aroy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marissa Aroy mnamo mwaka 2015

Marissa Aroy ni mwongozaji na mtayarishaji wa filamu wa Marekani mwenye asili ya Ufilipino. Aliongoza utayarishaji wa makala za Sikhs huko Marekani, ambazo zilipokea tuzo ya Emmy kwa "mpango bora wa historia", na The Delano Manongs. Pia Aroy ni mwanzilishi  wa kampuni ya uzalishaji filamu iitwayo Media Factory. Aroy hivi majuzi aliorodheshwa kama mmoja wa "Wamarekani wenye asili ya Asia mashuhuri  katika Burudani" na Kituo cha Habari cha Asian American na kutajwa na BuzzFeed kama mmoja wa "Wamarekani wenye asili ya Ufilipino maarufu zaidi nchini Marekani".[1]

Aroy alipata shahada yake ya kwanza ya Saikolojia katika Chuo cha Boston na akamalizia Shahada ya Uzamili ya Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha California,Berkeley. Kwa miaka miwili alafanyakazi katika kikosi cha amani katika Jamhuri ya Dominikana akifanya kazi katika sekta ya afya ya umma na kutengeneza filamu kuhusu VVU/UKIMWI katika Jamhuri ya Dominikana. Kama Msomi, Aroy alirekodi simulizi kuhusu athari za uhamiaji kwenye familia moja inayoitwa Recipe.[2][3][4]

  1. "Mutua uulnera: Dying Together in Silius' Saguntum", Family in Flavian Epic, BRILL, ku. 228–247, 2016-01-01, iliwekwa mnamo 2022-08-12
  2. Tan, Avianne. "Lea Salonga And 33 Other Epic Filipino-Americans Got Together For A Big Family Photo". www.buzzfeed.com (kwa Kiingereza).
  3. "Filmmaker Advice: Marissa Aroy". caamedia.org. 3 Oktoba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Nadal, Kevin. "Why We Celebrate Filipino American History Month".

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]