Margarita Bourgeoys

Margarita Bourgeoys, CND (17 Aprili 1620 - 12 Januari 1700[1]), alikuwa mtawa wa Ufaransa na mwanzilishi wa Shirika La Notre Dame wa Montreal katika koloni la New France, ambayo sasa ni sehemu ya Québec, Kanada.
Alitangazwa rasmi mwenyeheri na Papa Pius XII tarehe 12 Novemba 1950, halafu mtakatifu na Papa Yohane Paulo II 31 Oktoba 1982.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mzaliwa wa Troyes, alisafiri kwenda Fort Ville-Marie (sasa Montreal) mwaka 1653, ambapo aliendeleza kwa bidii kubwa mabinti wa wasomi, maskini, na Waindio hadi muda mfupi kabla ya kifo chake [3][4].
Kabla Bourgeoys hajapata kutambuliwa mnamo 1982 kama mtakatifu katika Kanisa Katoliki, watu wengi tayari waliamini kuwa alikuwa na sifa hiyo kwa jinsi alivyosaidia kwa kila njia wahamiaji. Siku iliyofuatia kifo chake, kuhani aliandika, "Ikiwa watakatifu wangetangazwa kama zamani na sauti ya watu na ya wachungaji, kesho tungekuwa tunasema Misa ya Mtakatifu Margarita wa Kanada." Helene Bernier aliandika, "Pongezi zake mara nyingi zilikuwa zimeshatangazwa miaka 250 kabla ya kutangazwa kwake mtakatifu."
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk 25-26
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 19-20
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |