Nenda kwa yaliyomo

Mapadri wa Betharram

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanzilishi alivyochorwa.

Mapadri wa Moyo Mtakatifu wa Yesu wa Betharram (kifupi: Mapadri wa Betharram) ni shirika la kitawa la Kanisa Katoliki.

Lilianzishwa na mtakatifu padri Mikaeli Garicoits (15 Aprili 1797 - 14 Mei 1863) mwaka 1838 huko Betharram, chini ya milima ya Pirenei, maili 8 kutoka Lourdes, kulikokuwa na patakatifu pa zamani pa Bikira Maria.

Mwaka 1833 askofu alifunga seminari ya Bétharram na padri Mikaeli aliachwa huko kuhudumia patakatifu na umati wa watu waliokwenda huko kuhiji.

Hivyo mwaka 1838 Michel aliweza kutimiza ndoto yake ya kuanzisha shirika la mapadri na mabradha lililowekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Lengo la kulianzisha lilikuwa kuinjilisha watu kwa kuhubiri huko na huko na kwa kufundisha vijana.

Mikaeli Garicoits alifariki tarehe 14 Mei 1863. Baada ya kifo chake, shirika lilikubaliwa na Papa Pius IX tarehe 5 Septemba 1877.

Mwaka 2012 lilikuwa na wanachama 316, kati yao mapadri 212.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  • Letter Of Pope John Paul II To The Priests Of The Sacred Heart Of Betharram, 5 July 1997
  • "Societas Presbyterorum Sacratissimi Cordis Iesu de Bétharram". Catholic Hierarchy.
  • Website
  • Saint Michael Garicoits
  • St. Michael Garicoits Archived 16 Februari 2002 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapadri wa Betharram kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.