Nenda kwa yaliyomo

Makumbusho ya Azimio la Arusha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
mnara wa Mwenge karibu na Makumbusho ya Azimio

Makumbusho ya Azimio la Arusha yanapatikana karibu kabisa na Mnara wa Mwenge eneo la Kaloleni jijini Arusha.

Mwaka 1967 jengo hilo lilitumika kwa mkutano wa kihistoria kuhusu sera za siasa na uchumi za Tanzania za ujamaa na kujitegemea zilizotolewa mwaka 1977 na kufanya jengo hilo kubadilishwa na kuwa makumbusho madogo ya kisasa [1] katika mkoa huo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Makumbusho ya Azimio la Arusha yalianza kutumika mwaka 1977 wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka kumi ya Azimio hilo, lakini kabla ya hapo jengo hilo lilikuwa likitumika kama ofisi za ustawi wa jamii kwa watu wa kata ya Kaloleni. Jengo hilo lilipata umaarufu zaidi tarehe 26 hadi 29 pala ambapo kamati kuu ya CCM ilikaa chini na kupendekeza sera ya taifa ya Ujamaa na Kujitegemea iliyotangazwa rasmi tarehe 5 Februari 1967 na Mwalimu Julius Nyerere [2]

Jengo hili lipo pembezoni mwa makutano ya barabara nne za Kaloleni na katikati yake pamejengwa mnara wa mwenge, juu yake kukiwa na mfano wa mwenge unaowaka.

Maonyesho[hariri | hariri chanzo]

Eneo hilo hutumika kufanya maonyesho mbalimbali ikiwemo matukio ya kabla ya ukoloni na baada ya uhuru, historia ya mapambano ya makabila ya Tanzania na wavamizi waliovamia maeneo yao enzi za zamani pamoja na mapambano ya Vita vya Kagera na historia ya hali ya kisiasa Tanzania.

Fursa nyingine[hariri | hariri chanzo]

Mbali ya maonyesho katika jengo hilo la makumbusho ya Azimo la Arusha, fursa nyingine hupatikana katika maeneo yake ikiwemo:

  • Maeneo ya nje kwa ajili ya maonyesho na sherehe
  • Vyumba kwa ajili ya semina na warsha
  • Ushirikiano wa kiutafiti
  • Ushauri wa Usimamizi wa urithi
  • Huduma za kutembeza ziara na mihadhara juu ya mada maalum juu ya utamaduni na historia

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-03. Iliwekwa mnamo 2020-03-11.
  2. https://www.ippmedia.com/sw/makala/azimio-la-arushachimbuko-la-mfumo-wa-tanzania-lililotelekezwa