Makinikia
Makinikia (Kiing. ore concentrate) ni jina la mchanganyiko wa madini, miamba na wakati mwingine kemikali ambao hutokana na shughuli za uchimbaji wa metali. Metali nyingi kama chuma, shaba au dhahabu hazipatikani kwa umbo safi lakini kama mtapo (ore) ndani ya miamba inayochimbwa. Mtapo unaopatikana ardhini huwa na asilimia kubwa ya miamba ambayo haina tija kiuchumi. Hivyo mtapo hupelekwa kwa kifaa cha kuponda ambapo sehemu yenye madini husika inatenganisha na sehemu isiyo na madini. Mbinu zinazotumiwa kutenganisha sehemu hizi ni pamoja na kutumia nguvu ya sumaku, graviti au kemikali. Matokeo yake ni makinikia ambamo kiwango cha metali ni kubwa kuliko katika mtapo uliochimbwa.
Makinikia inapelekwa hadi kiwanda ambako madini yake hutenganishwa zaidi na kusafishwa.
Jina
Neno hili limepata umaarufu na kutumiwa zaidi na Watanzania baada ya Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kugundua udanganyifu unaofanywa na makampuni mbalimbali ya uchimbaji madini nchini Tanzania ikiwamo kampuni ya Acacia Mining, kama ilivyofichuliwa na vyama vya upinzani tangu miaka ya nyuma.
Hali hiyo ilipelekea rais John Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa makanikia kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuuchambua ili kupata madini yaliyomo ndani yake. Badala yake aliingia katika mazungumzo na makampuni ya madini nchini Tanzania juu ya kurekebisha mikataba mbalimbali ya madini na kuyataka makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini kujenga mitambo (Smelter) ya kuchenjua mchanga huo nchini humo, si kuusafirisha kwenda nje ya nchi.[1][2][3][4] [5] [6] [7]
Marejeo
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-10-13. Iliwekwa mnamo 2017-10-28.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-10-13. Iliwekwa mnamo 2017-10-28.
- ↑ http://www.mwananchi.co.tz/habari/Mambo-manane-kutikisa-kikao-cha-makinikia/1597578-4041838-j3j36cz/index.html
- ↑ http://www.mwananchi.co.tz/habari/Ripoti-ya-makinikia-yaibua-uozo-wa-mikataba-ya-madini/1597578-3967788-6vpowm/index.html
- ↑ http://www.mwananchi.co.tz/habari/Ripoti-ya-makinikia-yaibua-uozo-wa-mikataba-ya-madini/1597578-3967788-6vpowm/index.html
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-09-18. Iliwekwa mnamo 2017-10-28.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-06-18. Iliwekwa mnamo 2017-10-28.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Makinikia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |