Makinikia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mmoja wa mitambo (smelter) ya kuchenjua mchanga wenye madini (makinikia).
Mmoja ya mitambo ya zamani ya kuchenjulia madini huko bandari ya Sagunto, Valencia, Hispania.

Makinikia (kutoka neno "makini") ni jina la mchanga ambao hutokana na shughuli za uchimbaji wa madini. Mchanga huo husadikika kuwa na madini ya aina moja ama zaidi ya madini ndani yake.

Neno hili limepata umaarufu na kutumiwa zaidi na Watanzania baada ya Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kugundua udanganyifu unaofanywa na makampuni mbalimbali ya uchimbaji madini nchini Tanzania ikiwamo kampuni ya Acacia Mining[1], kama ilivyofichuliwa na vyama vya upinzani tangu miaka ya nyuma.

Hali hiyo ilipelekea rais John Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga huo wenye madini kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuuchambua ili kupata madini yaliyomo ndani yake. Badala yake aliingia katika mazungumzo na makampuni ya madini nchini Tanzania juu ya kurekebisha mikataba mbalimbali ya madini na kuyataka makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini kujenga mitambo (Smelter) ya kuchenjua mchanga huo nchini humo, si kuusafirisha kwenda nje ya nchi.[2][3][4][5] [6] [7] [8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makinikia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.