Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Alex Leo Tz

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:46, 16 Februari 2022 (UTC)[jibu]

Asante Sana Alex Leo Tz (majadiliano) 10:31, 18 Februari 2022 (UTC)[jibu]
Ukurasa wa kwanza ulioanzisha haukulingana na maelekezo ya hapa juu. Uyasome vizuri na utaona suala la kutafsiri kwa mashine. Ukurasa wako haukueleweka kwa Mswahili. Pole na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:16, 2 Desemba 2023 (UTC)[jibu]
Asante kwa mrejesho ila hakuna sehemu yoyote niliyotumia programu za kutafsiri lugha
Changamoto ni kwamba kiswahili kina upungufu mkubwa wa msamiati haswa ya kisayansi na kiteknolojia
Mfano neno "Large language model" halina tafsiri yoyote ile ya kiswahili (Mimi ni mtanzania mzawa) na hakukua na kurasa yoyote ile Wikipedia ya kiswahili inayozungumzia LLM licha ya umuhimu wake mkubwa kwa sasa
Neno autoregressive halina tasfiri ya kiswahili, hio ni mifano michache ya maneno mengi mno ya kingereza ambayo hayapo kwenye kiswahili kabisa
Sasa tunapokuja kuandaa kurasa za taarifa ambazo zina misamiati michache kwenye kiswahili ni wazi inaweza onekana kama umetumia google translate au programu za namna hio, lakini si sahihi
Huwa na tafsiri neno kwa neno kulingana na kile kinachofahamika Alex Leo Tz (majadiliano) 15:05, 2 Desemba 2023 (UTC)[jibu]
Ndugu, hongera kwa hilo. Kutafsiri ni kazi ngumu daima, hasa katika baadhi ya fani. Ngoja nirudishe ukurasa wako ili uone namna ya kufanya ueleweke zaidi kwa mtu asiyejua Kiingereza. Lakini pia kuna Kamusi ya Sayansi na Teknolojia ambayo inaweza kusaidia kidogo, badala ya kuanza na moja. Amani kwako! Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:42, 3 Desemba 2023 (UTC)[jibu]
Asante sana kwa kurudisha ukurasa wa awali, nitajitahidi kadri ninavyoweza kueleweka Alex Leo Tz (majadiliano) 10:05, 4 Desemba 2023 (UTC)[jibu]
Usitafsiri sisisi. Tafsiri muktadha utapata maana. Je, ulivyosema "autoregressive" ulielewa nini? Ukielewa, ndiyo unapata maana ya Kiswahili. Muktadha sio neno kwa neno. Ukiendelea kutafsiri zaidi, unapata uwezo wa kupunguz urefu wa istilahi na tahajia. Kadhalika makala ya CHATGPT inahitaji usanifu mkubwa wa lugha. Ile ni tafsiri ya Kiingereza kuja Kiswahili. Tena ni neno kwa neno. Matokeo yake inapoteza maana. Nikitulia kesho nitajaribu kuiweka sawa. Karibu sana! Muddyb Mwanaharakati Longa 21:02, 12 Januari 2024 (UTC)[jibu]