Lyambamgongo
Lyambamgongo ni kata ya Wilaya ya Bukombe katika Mkoa wa Geita, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,314 waishio humo.[1] Msimbo wa posta ni 30502.[2]
Wakazi wengi wa maeneo haya ni Wasukuma na shughuli zao kuu ni kilimo, ufugaji na biashara itokanayo na mazao ya kilimo, misitu na mifugo.
Kijiji cha Lyambamgongo, ambacho ni makao makuu ya kata hiyo, kinapatikana takribani kilometa kumi kutoka Ushirombo yaliko makao makuu ya wilaya ya Bukombe katika barabara kuu ya lami iendayo Rwanda na Burundi kupitia Nyakanazi.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Sensa ya 2012, Geita Region – Bukombe District Council
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
![]() |
Kata za Wilaya ya Bukombe - Mkoa wa Geita - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Bugelenga | Bukombe | Bulangwa | Bulega | Busonzo | Butinzya | Igulwa | Iyogelo | Katente | Katome | Lyambamgongo | Namonge | Ng'anzo | Runzewe Magharibi | Runzewe Mashariki | Ushirombo | Uyovu |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |