Ludoviko wa Toulouse
Mandhari
(Elekezwa kutoka Ludoviko wa Tolosa)
Ludoviko wa Toulouse (Brignoles, Provence, Ufaransa, Februari 1274 - Toulouse 19 Agosti 1297) alikuwa mwana wa mfalme wa Napoli Charles II wa Anjou, mdogo wake Ludoviko IX, lakini akitamani ufukara wa Kiinjili kuliko sifa na heshima za kidunia, alikataa haki ya kumrithi akawa mtawa wa Ndugu Wadogo na askofu wa Kanisa Katoliki mjini Toulouse[1].
Akiwa kijana kwa umri lakini mkomavu katika maadili alifariki mapema kutokana na afya wake dhaifu[2].
Alitangazwa na Papa Yohane XXII kuwa mtakatifu tarehe 7 Aprili 1317.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90385
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90385
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholic Encyclopedia: St Louis of Toulouse
- Amelia Carr, "St Louis of Toulouse" Ilihifadhiwa 8 Julai 2004 kwenye Wayback Machine.
- Patron Saints: Louis of Toulouse Ilihifadhiwa 30 Juni 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |