Luanda
Jiji la Luanda | |
Nchi | Angola |
---|
Luanda (kirefu: São Paulo de Luanda: pia Loanda) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Angola ikiwa na wakazi 2,487,484 (katika rundu la jiji 7,805,000) wanaongezeka haraka kutoka ndani na nje ya nchi na ya bara la Afrika.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Mji wa Luanda uko mkoani Luanda, kaskazini ya mdomo wa mto Cuanza mwambaoni pa Atlantiki.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mji ulianzishwa na Wareno mwaka 1575 BK kwa jina la São Paulo de Luanda. Umekuwa mji mkuu wa Angola tangu mwaka 1627.
Hadi mwaka 1850 Luanda ilikuwa kitovu cha biashara ya watumwa kwenda Brazil.
Wakati wa uhuru mwaka 1975 walowezi wengi Wareno waliondoka mjini. Vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Angola kati ya miaka 1974 - 2002 ilileta hasara pia kwa mji mkuu.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Kati ya wakazi, walio wengi kabisa ni Waafrika wa makabila kama vile Waovimbundu, Wakimbundu na Wakongo.
Lugha rasmi ni Kireno lakini lugha nyingi za Kibantu zinatumika pia.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Luanda ni bandari muhimu nchini pia mwanzo wa reli kwenda Malange.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- www.luandamap.com - Ramani ya Luanda Archived 17 Mei 2019 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Angola bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Luanda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |