Nenda kwa yaliyomo

Loki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Loki kwenye muswada wa Iceland mnamo karne ya 18.

Loki ni mungu mmojawapo katika masimulizi ya mitholojia ya Skandinavia ya kale au kwa lugha nyingine mitholojia ya mataifa ya Wagermanik ya Kaskazini.

Katika mitholojia hiyo alikuwa mwana wa majitu wawili aliyepokewa katika nasaba ya miungu ya Asgard. Alikuwa na uwezo wa kutokea kwa maumbo tofautitofauti, mara kama samaki, mara kama nzi. Alikuwa na akili kubwa na pamoja na uwezo wake wa kubadilisha umbo alipata sifa kama kielelezo wa ushabaki na hila. Alisemekana pia kuwa mzazi wa madubwana mbalimbali.

Mwishoni alisababisha kifo cha mungu Balder mwana wa miungu mikuu Odin na Frigga. Hivyo alijipatia uadui wa miungu wengine wa Asgard waliofaulu kumshinda na kumwua.

Katika fasihi ya kisasa Loki ni mhusika katika katuni za Marvel Comics pamoja na filamu zao.