Lindi (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Lindi
Lindi is located in Tanzania
Lindi
Lindi
Mahali pa mji wa Lindi katika Tanzania
Majiranukta: 9°59′49″S 39°42′52″E / 9.99694°S 39.71444°E / -9.99694; 39.71444
Nchi Tanzania
Mkoa Lindi
Wilaya Lindi Mjini

Lindi ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Lindi. Lindi iko mdomoni wa mto Lukuledi takriban 150 km kaskazini ya Mtwara mwambaoni wa Bahari Hindi. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 41,549 [1]

Lindi ilikuwa kati ya miji ya Waswahili kwenye pwani la bahari. Mdomo wa Lukuledi ilikuwa bandari nzuri kwa ajili ya jahazi za Waswahili na pia kwa meli ndogo za zamani za ukoloni. Siku hizi haitoshi tena kwa meli kubwa.

Wakati wa ukoloni wa Wajerumani ilikuwa makao makuu ya kusini-mashariki ya Tanzania bara. Ilikuwa kituo cha Posta na pia cha kikosi na. 3 cha jeshi la Kijerumani. Ilibaki kitovu cha eneo chini ya Waingereza hadi kujengwa kwa bandari ya Mtawara. Mazao ya kibiashara yalikuwa hasa katani baadaye pia korosho.

Maendeleo ya Lindi ilikwama kutokana na hali mbaya za barabara amabazo hazikutunzwa vizuri wakati wa uhuru. Kuna matumaini ya kwamba mipango ya barabara ya lami ya Dar es Salaam - Mtwara itandelea baada ya kukamilika kwa daraja la mto Rufiji.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lindi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Lindi Mjini - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chikonji | Jamhuri | Kitumbikwela | Makonde | Matopeni | Mbanja | Mikumbi | Mingoyo | Mitandi | Mnazimoja | Msanjihili | Mtanda | Mwenge | Nachingwea | Ndoro | Ng'apa | Rahaleo | Rasbura | Tandangongoro | Wailesi|}