Rutamba
Rutamba ni kata iliyopo Manispaa ya Lindi, Mkoa wa Lindi, kusini mwa Tanzania.
Kijiografia, kata ya Rutamba inapatikana takriban kilomita 40 magharibi mwa mji wa Lindi.
Msimbo wa posta ni 65208.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 12,801 [1]. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka wa 2012, kata ya Rutamba ilikuwa na wakazi wapatao 11,210[2].
Wakati Rutamba ni kata, kwa upande mwingine ni kijiji kinachojitegemea ambacho ndani yake kuna vitongoji vinne ambavyo ni: Rutamba ya Zamani, Rutamba ya Sasa, Michee na Chilala. Pamoja na hivyo ambavyo vipo ndani ya mipaka ya kijiji cha Rutamba, pia kuna vijiji vya Kinyope, Makangara, na Ruhoma ambavyo kwa pamoja vinaunda Kata ya Rutamba.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz/
- ↑ "Sensa ya 2012, Lindi - Lindi DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-22.
Kata za Wilaya ya Lindi Mjini - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Chikonji | Jamhuri | Kilangala | Kilolambwani | Kitomanga | Kitumbikwela | Kiwawa | Makonde | Matimba | Matopeni | Mbanja | Mchinga | Mikumbi | Milola | Mingoyo | Mipingo | Mitandi | Mnazimmoja | Msinjahili | Mtanda | Mvuleni | Mwenge | Nachingwea | Nangaru | Ndoro | Ng'apa | Rahaleo | Rasbura | Rutamba | Tandangongoro | Wailes
|