Lukuledi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa Lukuledi (maana)

Picha:Flußbett des Lindiflusses während der Ebbe Deutsch-Ostafrika.jpg
Mdomo wa mto Lukuledi karibu na Lindi kwenye kiangazi wakati wa maji kupwa

Mto Lukuledi unaingia katika Bahari Hindi kwenye mji wa Lindi. Lukuledi ina urefu wa takriban 160 km. Wakati wa ukame maji si mengi lakini kwenye 40 km za mwisho kabla ya mdomo maji hupatikana. Kwenye 20 km za mwisho kabla ya mdomo mto hupanuka kuwa hori ya bahari.

Bonde la Lukuledi hutenganisha nyanda za juu za Makonde na bonde za juu za Muera.