Liberata Mulamula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Liberata Mulamula


Waziri ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Rais Samia Suluhu Hassan
mtangulizi Palamagamba Kabudi

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Meksiko
Rais Jakaya Kikwete
mtangulizi Mwanaidi Maajar

Mshauri wa rais
(Diplomasia)
Rais Jakaya Kikwete

Katibu Mtendaji wa ICGLR
aliyemfuata Ntumba Luaba

Balozi wa Tanzania nchini Kanada
Rais Benjamin Mkapa

utaifa Tanzanian
ndoa George
watoto 2
mhitimu wa Chuo Kikuu cha St. John's (New York City) (MA)
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Liberata Mulamula (amezaliwa 10 Aprili 1956) ni mwanadiplomasia wa Tanzania na tangu Machi 2021 waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki[1]. Tangu mwaka 2015 alihudumia kama katibu mkuu wa wizara hiyo[2]. Aliwahi kuwa balozi wa Tanzania katika Marekani pamoja na Meksiko [3] [4], aliwakilisha Tanzania pia kwenye Umoja wa Mataifa pamoja na Kanada na kati ya miaka 2006–2011 alikuwa katibu mtendaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanda la Maziwa Makuu ya Afrika[5].

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Liberata Rutageruka alizaliwa huko Muleba, mkoa wa Kagera. [6]

Alihitimu shahada ya uzamili katika somo la siasa kwenye Chuo Kikuu cha St. John’s, New York mwaka 1980 na pia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo 1989.

Ameolewa na George Mulamula na ana watoto wawili, Tanya na Alvin.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 

  1. ‘Sura’ tatu za uteuzi wa balozi Mulamula, gazeti la Mwananchi 02.04.2021
  2. Balozi Mulamula. Michuzi Blog (4 May 2015). Iliwekwa mnamo 4 May 2015.
  3. Kikwete picks new envoys (May 15, 2013). Jalada kutoka ya awali juu ya July 13, 2013. Iliwekwa mnamo August 8, 2013.
  4. Ambassador’s Biography. Tanzaniaembassy-us.org. Embassy of Tanzania, Washington, D.C. (July 2013). Jalada kutoka ya awali juu ya August 1, 2013. Iliwekwa mnamo August 8, 2013.
  5. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-08-23. Iliwekwa mnamo 2021-04-02.
  6. Alumni of the Month: Liberata Rutageruka Mulamula, University of Dar es Salaam.