Leleti Khumalo
Leleti Khumalo | |
---|---|
Amezaliwa | 1970 Durban, South Africa |
Miaka ya kazi | 1988 hadi sasa |
Leleti Khumalo (alizaliwa KwaMashu, kaskazini mwa Durban, Afrika Kusini, 1970) ni mwigizaji mwenye asili ya Zulu wa Afrika Kusini ambaye alicheza nafasi ya kuongoza katika filamu ya Sarafina! sambamba na Whoopi Goldberg na aliyeigiza katika filamu za Hotel Rwanda na Yesterday .
Baada ya kuonyesha nia ya kuigiza kuanzia umri mdogo, Khumalo alijiunga na kundi la vijana la kukcheza iitwayo Amajika, iliyoongozwa na Tu Nokwe.
Sarafina!
[hariri | hariri chanzo]Katika 1985, alijaribu kuigiza katika kimuziki cha Mbongeni Ngema, ambayo baadaye ikawa filamu kubwa ya kimataifa ya Sarafina!, Ngema aliiandika sehemu ya uongozi ya Sarafina hasa kwa Khumalo. Sasa ameolewa na Mbongeni Ngema. Lakini kumekuwa na madai kwamba yeye amekuwa na mahusiano kadhaa na wanawake tofauti, ikiwa ni pamoja na marehemu Brenda Fassie.
Khumalo aliigiza sehemu ya Sarafina! katika jukwaa Afrika ya Kusini na Broadway, ambapo alipewa Tuzo la Tony 1988 la Muigizaji Bora zaidi wa Kike katika filamu ya kimuziki. Sarafina! ilikaa Brodway kwa muda wa miaka miwili, na baadaye wakaanza ziara ya dunia mzima. Mwaka 1987 alipata tuzo la NAACP la Muigizaji bora zaidi wa kike.
Mwaka 1992, alishirikiana sambamba na Whoopi Goldberg, Miriam Makeba na Yohana kani katika filamu ya Darrell James Roodt ya Sarafina Ambayo ilikuwa filamu kubwa zaidi kutolewa Barani Afrika. Kwa mara nyingine, Khumalo aliteuliwa kwa tuzo la Image pamoja na Angela Bassett, Whoopi Goldberg na Janet Jackson.
Iliyoigizwa kulingana na fujo za vijana katika mji wa Soweto mwaka 1976, Sarafina inaelezea hadithi ya msichana wa shule ambaye haogopi kupigania haki zake na kuwahamasisha wenzake kusimama katika maandamano, hasa baada ya mwalimu wake, Maria Masembuko (Whoopi Goldberg) kutiwa mbaroni.
Mwaka 1993, Khumalo alitoa albamu yake ya kwanza, Leleti and Sarafina
Sarafina! ilitolewa tena Afrika Kusini tarehe 16 Juni 2006 kama ukumbuzi wa 30 wa fujo za vijana za Soweto.
Kazi za baadaye
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa muigizaji msaidizi katika filamu ya muziki ya Mbongeni Ngema ya Magic at 4 AM ambayo ilikuwa wakfu wa Muhammad Ali. Alikuwa muigizaji mkuu katika filamu nyingine ya Ngema, Mama (1996), ambayo ilifanya ziara ya Ulaya na Australia. Mwaka 1997, aliigiza pia katika Sarafina 2.
Khumalo aliigiza katika filamu za mwaka wa 2004 za Hotel Rwanda na Yesterday , ambazo Yesterday iliteuliwa kupata tuzo la Academy Award 2005 katika kitengo cha "Filamu bora zaidi isiyo ya kiingereza". Yesterday pia hivi karibuni ilipata tuzo la Filamu bora Zaidi katika masherekeo ya Kimataifa ya Filamu ya India ya Pune na ilipokelewa vizuri katika masherekeo ya Kimataifa ya Filamu ya Venice na Toronto.
Khumalo alijiunga waigizaji wa kipindi kinachoendelea zaidi cha Afrika ya Kusini cha Generations mwaka 2005 kama Busiswe (Busi) Dlomo. Ametumia akili yake kufika aliko leo, katika uongozi wa kampuni ya mawasiliano ya Afrika ya Kusini, Ezweni, ambayo anamiliki yeye na kaka yake na mwanzilishi Karabo Moroka.[1]
Filamu
[hariri | hariri chanzo]- Invictus (2009) .... Mary
- Faith's Corner (2005) .... Faith
- Hotel Rwanda (2004) .... Fedens
- Yesterday (2004) .... Yesterday
- Cry, the Beloved Country (1995) (kama Leleti Kumalo) .... Katie
- Sarafina! (1992) .... Sarafina
- Voices of Sarafina! (1988)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-07-21. Iliwekwa mnamo 2021-01-17.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Leleti Khumalo kwenye Internet Movie Database
- Picha za Khumalo katika filammu Yesterday Archived 7 Februari 2012 at the Wayback Machine.
- Wasifu wa Generations wa Khumalo Archived 21 Julai 2006 at the Wayback Machine.