Lava (volkeno)
Lava (kutoka jina la Kiingereza lenye asili ya Kilatini lava, wakati mwingine pia zaha[1]) ni mwamba ulio katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa dunia mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "magma" badala ya lava. Sawa na magma yenyewe lava inaweza kuwa nzito kama ujiuji au nyepesi kama majimaji.[2] .
Lava inatoka nje kwa kawaida wakati wa mlipuko wa volkeno. Inaweza kutoka pia katika ufa kwenye ganda la dunia.
Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600°C hadi 1200°C. Ndani ya shimo la kasoko ya volkeno lava inaweza kukaa kama ziwa la kuchemka.
Ikitoka nje ya kasoko inaweza kuwa kama mto wa moto. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.
Ikipoa inaganda na kuwa mwamba imara.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mlipuko wa volkeno ya Stromboli (Italia) - kile chekundu kwenye picha ni lava.
-
Mto wa lava kwenye volkeno ya Kilauea (Hawaii)
-
Lava ikipoa inaweza kuonekana hivyo.
-
Ziwa la lava ndani ya kasoko ya mlima Nyiragongo huko Goma (Kongo)
-
Mto wa lava inavyoharibu nyumba huko Hawaii mwaka 1990
-
Mita kumi kwenda juu(33 ft) Chemchemi ya lava huko Hawaii, Marekani
-
Lava ikitiririka wakati wa mlipuko wa ufa huko Krafla, Iceland mwaka wa 1984
-
Pāhoehoe na ʻaʻā lava hutiririka pamoja huko Hawaii, Septemba 2007
-
Uunganishaji wa safu wima katika Giant's Causeway huko Ireland Kaskazini
-
Lava ikiingia baharini kupanua kisiwa kikubwa cha Hawaii, Hawaii Volcanoes National Park
-
Lava ikiingia Pasifiki katika Kisiwa Kikubwa cha Hawaii
-
Lava ya Pāhoehoe kutoka kwenye volkano ya Kīlauea,Hawaii,Marekani
-
katika Hifadhi ya taifa ya Volcanic ya Lassen
-
Pillow lava kwenye sakafu ya bahari karibu na Hawaii]]
-
Arenal Volcano, Costa Rica, ni stratovolcano.
-
Kuba la lava lenye msitu katikati ya Valle Grande, mbuga kubwa zaidi katika Hifadhi ya Taifa ya Valles Caldera, Mexico Mpya, Marekani.
-
Shiprock, Mexico Mpya, Marekani, shingo ya volkeno kwa mbali, yenye lambo inayoangaza upande wake wa kusini.
-
Urefu wa mita 450 wa chemchemi ya lava huko Kilauea
-
Ziwa ya lava kwenye Mlima Nyiragongo katika [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kamusi za TATAKI na BAKITA hutaja zaha kama visawe vya lava; kamusi ya KAST inataja zaha kama visawe vya volkeno yenyewe.
- ↑ Earth Science. Holt, Rinehart and Winston, Austin, Texas. 2001. ISBN 0-03-055667-8.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help)
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lava (volkeno) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |