Mweru (ziwa)

Majiranukta: 9°00′S 28°43′E / 9.000°S 28.717°E / -9.000; 28.717
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lake Mweru)
Mweru (ziwa)
Southern end of the lake from space, June 1993 (false color)
Anwani ya kijiografia 9°00′S 28°43′E / 9.000°S 28.717°E / -9.000; 28.717
Aina ya ziwa Maziwa ya Bonde la Ufa
Mito ya kuingia Luapula (mto)
Kalungwishi (mto)
Mito ya kutoka Luvua (mto)
Nchi za beseni Zambia
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Urefu 131 km
Upana 56 km
Eneo la maji 5,120 km² (1,977 sq. mi.)
Kina cha wastani 7.5 m
Kina kikubwa 27 m
Mjao 38.2 km³
Urefu wa pwani (km) 436 km
Kimo cha uso wa maji juu ya UB 917 m
Visiwa Kisiwa cha Kilwa
Kisiwa cha Isokwe
Miji mikubwa ufukoni Nchelenge, Kashikishi, Chiengi, Pweto, Kilwa, Lukonzolwa
1 Shore urefu is not a well-defined measure.

Ziwa Mweru (pia Mwelu, Mwero) ni ziwa kubwa mpakani mwa Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni sehemu ya mfumo wa mto Kongo kati ya mto Luapula (upande wa juu) na mto Luvua (chini yake).[1]

Jina Mweru lamaanisha 'ziwa' kwa lugha mbalimbali za Kibantu.[2]

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mweru inapokea maji yake hasa kutoka mto Luapula unaoingia upande wa kusini halafu kutoka mto Kalungwishi unaoingia upande wa mashariki. Upande wa kaskazini maji yake yanatoka kupitia mto Luvua unaoingia katika mto Lualaba na kutoka huko kwenye mto Kongo.

Ni ziwa kubwa la pili katika beseni ya Kongo likifunika kwa wastani eneo la km² 5,120. Mweru iko kilomita 150 upande wa magharibi wa ziwa Tanganyika.[1].

Urefu wa ziwa ni kilomita 118 na upana wake km 45 likielekea kutoka kaskazini mashariki kwenda kusini magharibi. Uso wa ziwa uko mita 917 juu ya UB kwa hiyo uko juu kuliko Ziwa Tanganyika kwa m 763. Ni moja ya maziwa ya bonde la ufa likiwa katika mkono wa pembeni wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.[3] Mwambao wa magharibi ni mtelemko mkali jinsi ilivyo mara nyingi kwenye maziwa ya bonde la ufa unaopaa hadi milima ya Kundelungu.

Kina ni kirefu upande wa kaskazini kinapofikia mita 27.

Makazi ya watu ziwani[hariri | hariri chanzo]

Kuna vijiji vingi vya wavuvi kwenye mwambao. Miji upande wa Zambia ni Nchelenge, Kashikishi na Chiengi halafu [Kilwa (Katanga)|Kilwa]] (ng'ambo ya kisiwa), Lukonzolwa na Pweto upande wa J D Kongo.

Pamoja na kisiwa cha Kilwa kuna visiwa viwili vngine vinavyokaliwa na watu ambavyo ni Isokwa wa Zammbia (km² 3) na kisiwa kimoja upande wa Kongo chenye eneo la km² 2.

Wakazi upande wa Kongo waliathiriwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka 1999-2003.

Uvuvi[hariri | hariri chanzo]

Samaki wya Haplochromis moeruensis (Boulenger, 1899) kutoka Ziwa Mweru

Mweru ina samaki wengi aina ya tilapia wanaoitwa pale kwa Chibemba. Wanakaushwa kwenye jua na kufungwa katika vikapu kwa kuuzwa sokoni.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Google Earth accessed 29 March 2007.
  2. The Northern Rhodesia Journal online at NZRAM.org: J B W Anderson: "Kilwa Island and the Luapula." Vol II, No. 3 pp87–88 (1954)
  3. P Master, P. Dumont and H. Ladmirant: "Age Constraints On The Luizi Structure". 64th Annual Meteoritical Society Meeting. (2001). Accessed 30 March 2007.