Nenda kwa yaliyomo

Bonde la Ufa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bonde la ufa)
Mfano wa Bonde la Ufa ni nafasi ya Ziwa Tanganyika

Bonde la Ufa kwenye fani ya jiolojia ni bonde ambalo limetokana na mwendo wa mabamba ya gandunia mahali yanapoachana.

Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki ni mojawapo kati ya mabonde maarufu zaidi duniani.

Mabonde ya ufa hutokana na mvutano wa tektoniki. Mwendo huu huleta utengano wa mabamba hayo. Bonde la ufa latokea kama mabamba ya gandunia huachana na kuacha nafasi.

Mabonde ya ufa ni mahali ambako volkeno pamoja na matetemeko ya ardhi hujitokeza.

Mabonde ya ufa makubwa kabisa yapo chini ya maji kwenye misingi ya bahari.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.