Nenda kwa yaliyomo

Los Angeles

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka La)








Jiji la Los Angeles

Bendera
Nchi Marekani
Jimbo California
Wilaya Los Angeles
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 3,849,378
Tovuti:  www.lacity.org
L.A. mjini usiku
Kitovu cha L.A.
Ramani ya Los Angeles

Los Angeles (mara nyingi kifupi L.A.) ni mji wa Kalifornia ya kusini. Ni mji mkubwa kuliko yote ya Kalifornia na mji mkubwa wa pili wa Marekani mwenye wakazi 3,847,400 mjini penyewe na hadi milioni 18 katika rundiko la mji. Mji uko kando la Pasifiki katika tambarare kati ya bahari na milima.

Mtaa maarufu mjini Los Angeles ni eneo la Hollywood.

Wakazi wa jiji ni mchanganyiko wa watu kutoka pande zote za dunia. Takriban theluthi moja hawakuzaliwa Marekani bali walihamia hapa ni watu kutoka nchi 140 za dunia. Karibu nusu huongea Kihispania kama lugha ya mama; wengi kati hao kutoka familia wa wahamiaji kutoka Meksiko au nchi mbalimbali za Amerika Kusini. Wahamiaji wengine wametoka hasa Asia ya Mashariki kama vile China, Korea na Japani.

Wakazi asilimia 46.9% huhesabiwa kama Wazungu, 11.24% Waamerika Weusi na 10.0% Waasia, wengine wa vikundi mbalimbali. 42.2% husema Kiingereza kama lugha ya kwanza, 41.7% Kihispania, 2.4% Kikorea, 2.3% Kitagalog, 1.7% Kiarmenia, 1.5% Kichina na 1.3% Kiajemi.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Tangazo la Hollywood mjini L.A.

Jina la Los Angeles latoka katika lugha ya Kihispania likimaanisha "malaika"; ni kifupi cha jina la awali "El Pueblo de Nuestra Señora la Reina de los Ángeles del Río de Porciúncula" yaani "Kijiji cha Mama Yetu Malkia wa Malaika wa Mto Porsyuncula"; maana yake ni kwamba kijiji kiliwekwa wakfu kwa Bikira Mariamu kilipoundwa mwaka 1781 na mapadri Wafransisko walioinjilisha kwanza sehemu hiyo. Wakati ule Kalifornia ilikuwa bado chini ya Hispania kama sehemu ya Ufalme mdogo wa Hispania Mpya ambao baadaye ukawa Jamhuri ya Meksiko.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: