Kwediyamba
Kwediyamba ni kata ya Wilaya ya Handeni Mjini katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,182 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi zaidi ya 5,000 waishio humo.
Msimbo wa posta ni 21831[2].
Kata ya Kwediyamba inapatikana kusini magharibi mwa mji wa Chanika.
Ni eneo ambapo mnada wa Nderema ambao ni gulio kubwa la mifugo hufanyika siku ya Jumamosi.
Kata ya Kwediyamba inaundwa na vijiji vya Kwediyamba, Kwedizando, Tuliani, Kweinkambala na Mpakani. Pia ina shule mbili za msingi na Shule moja shikizi pamoja na shule moja ya sekondari inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa 2021.
Wakati wa mvua kata hiyo inakuwa na changamoto kubwa ya usafiri kuunganisha vijiji vyake pale mto Msangazi unapojaa maji kupita kiasi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "TCRA postcode list". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-02. Iliwekwa mnamo 2020-11-17.
Kata za Wilaya ya Handeni Mjini - Mkoa wa Tanga - Tanzania | ||
---|---|---|
Chanika | Kideleko | Konje | Kwamagome | Kwediyamba | Kwenjugo | Mabanda | Malezi | Mdoe | Mlimani | Msasa | Vibaoni |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kwediyamba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |