Kunene (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kunene (Cunene) ni mto wa Afrika ya kusini-Magharibi. Chanzo chake kiko Angola katika Nyanda za Juu za Bie inaelekea kusini hadi kufikia mpaka wa Namibia kwenye na mji wa Ruacana.

Kuanzia hapa mto ni mpaka kati ya Angola na Namibia hadi kufika Atlantiki. Mdomo wa mto baharini ni delta yenye upana wa 30 km. Mwendo wote ni wa 1207 km, beseni ina 109,832 km².

Kunene ina maporomoko huko Ruacana pia Epupa.

Serikali ya Namibia ilipanga kutengeneza lambo kwenye maporomoko ya Epupa. Mipango hii imepingwa vikali kwa sababu inaonekana kuhatarisha ekolojia ya eneo pamoja na hali ya maisha ya Wahima walio wenyeji.

Jina la mto unarudia katika jina la mkoawa Namibia wa Kunene.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]