Nenda kwa yaliyomo

Ktesiphon

Majiranukta: 33°5′37″N 44°34′50″E / 33.09361°N 44.58056°E / 33.09361; 44.58056
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

33°5′37″N 44°34′50″E / 33.09361°N 44.58056°E / 33.09361; 44.58056

Taq Kasra au maghofu ya jumba la Ktesiphon, upinde katikati, picha ya mwaka 1864.
Ramani ya Seleukia na Ktesiphon wakati wa Kiajemi; ramani inaonyesha njia mbalimbali zilizotumiwa na mto Hidekeli katika historia

Ktesiphon ulikuwa mji wa kale katika Mesopotamia uliopatikana kwenye ukingo wa mashariki wa mto Hidekeli, karibu kilomita 35 kusini mashariki mwa Baghdad ya leo.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ktesiphon ulikuwa mji mkuu wa kifalme wa milki ya Uajemi ya Kale (Iran) wakati wa nasaba za Waparthi na Wasasani kwa zaidi ya miaka mia nane hadi uvamizi wa Kiislamu wa milki ya Uajemi. Ktesiphon ulikuwa mji mkuu ingawa ulikuwa nje ya Uajemi yenyewe; lakini ilikuwa katikati ya maeneo ya rutuba ya Mesopotamia ambako kilimo kilileta kodi nyingi ambazo wafalme wa Uajemi walitegemea kwa utawala wao.

Ktesiphon katika karne za kuwa mji mkuu ulipanuka hadi kuunganishwa na mji wa Seleukia upande mwingine wa mto Hidekeli. Mara nyingi inatajwa kama "Seleukia-Ktesiphon". Mwishoni mwa karne ya 6 na mwanzoni mwa karne ya 7, iliorodheshwa kama jiji kubwa zaidi duniani.[1]

Wakati wa vita kati ya Dola la Roma na Uajemi, Ktesiphon ilitekwa mara tatu na Waroma. Baada ya uvamizi wa Waislamu mji huo ulishuka na wakazi waliondoka, kwa sababu nafasi yake kama kitovu cha utawala na uchumi ilichukuliwa na mji mpya, Baghdad.

Kati ya maghofu ya mji wa kale yako hasa mabaki ya jumba la kifalme yanayojulikana kama Taq Kasra. [2]

  1. "Largest Cities Through History". geography.about.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-18. Iliwekwa mnamo 25 Novemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Eventually no less than four Sasanian rulers were quoted as its builders: Shapur I (241–273), Shapur II (310–379), Chosroes I Anushirvan (531–579) and Chosroes II Parvez (590–628). Kurz, Otto (1941). "The Date of the Ṭāq i Kisrā". The Journal of the Royal Asiatic Society of Great Britain and Ireland. (New Series). 73: 37–41. doi:10.1017/S0035869X00093138. JSTOR 25221709.

 

Bibliografia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]