Nenda kwa yaliyomo

Konstantino wa Murom

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Konstantino akiwa kijana nyuma ya wazazi wake mwaka 1073.

Konstantino wa Murom (kwa Kirusi: Святой Блаженный Князь Константин; alifariki mwaka 1129) alikuwa mtoto wa mfalme Svyatoslav II wa Kiev na mjukuu wa Vladimir I.

Alimuomba baba yake atawala mji wa Murom, ili kuingiza katika Ukristo wazazi wake waliokuwa Wapagani.[1]

Kazi hiyo ilishindikana mpaka alipowaonyesha picha takatifu ya Mama wa Mungu: hapo walisujudu.[2] Kwa msaada wake, mwanae Fyodor aliendeleza umisionari katika eneo lote la kandokando.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Mei.[3]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.