Kizz Daniel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kizz Daniel
Jina Kamili Oluwatobiloba Daniel Anidugbe
Jina la kisanii Kizz Daniel
Nchi Nigeria
Aina ya muziki Afropop, Pop, R&B
Kazi yake Mwanamuziki
Miaka ya kazi 2014 - hadi leo

Oluwatobiloba Daniel Anidugbe (anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Kizz Daniel; amezaliwa Mei 1, 1994) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Nigeria. Alifahamika zaidi kwa nyimbo zake Woju na Yeba.

Alipoanza muziki alitambulika kwa jina la Kiss Daniel kabla ya kulibadilisha jina hilo Mei 2018.[1] Alitia saini mkataba wa rekodi na lebo ya G-Worldwide Entertainment mnamo 2013, lakini aliondoka kwenye lebo hiyo kufuatia mzozo wa mkataba uliotangazwa na mahakama.

Alianzisha lebo yake ya Fly Boy Inc mnamo Novemba 2017.[2]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Oluwatobiloba Daniel Anidugbe huko Abeokuta, jimbo la Ogun, Nigeria.[3]

Alihudhuria shule ya Abeokuta Grammar School na kuhitimu katika chuo kikuu cha Federal University of Agriculture, Abeokuta mnamo 2013, na kupokea shahada ya usimamizi wa rasilimali za maji na uhandisi wa maji. Akiwa chuoni aliamua kujihusisha na muziki kama taaluma.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Mei 2015, Kizz Daniel alitoa wimbo wa tatu Laye katika siku yake ya kuzaliwa, na wiki mbili baadae alitoa video zake ambazo zilichukuliwa sehemu za Afrika Mashariki na kuongozwa na AJE FILMS.

Daniel alitoa albamu yake ya kwanza itwayo New Era mnamo Mei 14, 2016.

Baada ya kuondoka kwenye lebo yake ya zamani ya G-WorldWide, alienda kuanzisha lebo yake binafsi FLYBOY I.N.C. ambayo kwa sasa inasimamia wasanii wawili Demmie Vee na Philkeyz. Kizz Daniel alishirikishwa kwenye wimbo wa Demmie Vee unaoitwa You Go Wait?.[4]

Mnamo tarehe 30 Disemba 2018, Daniel alitoa albamu yake ya pili na ya kwanza chini ya lebo yake FlyBoy Inc iliyoitwa No Bad Songz. Albamu hiyo ilikuwa na nyimbo 20 ikiwa ni pamoja na One Ticket ambayo alimshirikisha Davido. Wengine aliowashirikisha kwenye albamu hiyo ni pamoja na Nasty C, Diamond Platnumz, Philkeyz, Demmie Vee, Dj Xclusive, Wretch 32, Diplo na Sarkodie. Albamu hiyo kwa mara ya kwanza ilishika namba 55 kwenye chati ya iTunes ya Marekani na kuwa nambari 1 kwenye chati ya Albamu duniani ndani ya saa 24 baada ya kutolewa.

Mnamo tarehe 25 Juni 2020, alitoa albamu yake ya tatu iliyoitwa King of Love.[5]

Kukamatwa[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 8 Agosti 2022, Kizz Daniel alishikiiliwa na polisi jijini Dar es salaam, Tanzania kwa kushindwa kutumbuiza, hafla iliyoandaliwa na moja ya kampuni ya kitanzania ijulikanayo kama State of Vybes.[6]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu za studio na EP

  • New Era (2016)
  • No Bad Songz (2018)
  • King of Love (2020)
  • Barnabas (2021

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kiss Daniel changes name to Kizz Daniel". Bella Naija (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-05-29. 
  2. "CONFIRMED: Kiss Daniel Exits G-Worldwide and Unveils New Record Label". Nigerian Entertainment Today (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-17. Iliwekwa mnamo 2017-11-17. 
  3. "Kizz Daniel: Oluwatobiloba Daniel Anidugbe born triplets but one die". BBC News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-14. 
  4. "Demmie Vee Ft. Kizz Daniel – You Go Wait? [Music]". Mp3 Bullet (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-10. 
  5. "Kizz Daniel releases new album, 'King of Love'". Pulse Live (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-06-26. 
  6. "Kizz Daniel arrested in Dar Es Salaam, Tanzania over failure to perform". Off blog media.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-12. 
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kizz Daniel kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.