Chati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Chati
Chati mabega-meupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Muscicapidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
Fleming, 1822
Ngazi za chini

Jenasi 5:

Chati ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Muscicapidae. Sikuhizi wataalamu wengi wanaainisha spishi za Thamnolaea katika Myrmecocichla. Chati hawana rangi kali isipokuwa spishi za Thamnolaea ambao wana tumbo jekundu. Wengine ni weusi wengine wana rangi ya kijivu au kahawa. Spishi hizi zinatokea Afrika na kadhaa zinatokea Asia ya Magharibi mpaka Uhindi. Kwa kawaida huonekana juu ya miwamba, majabali na vilima vya mawe. Hula wadudu, matunda madogo, mafuta ya wanyama na takataka za kulika za nyumba. Hulijenga tago lao kwa vitu vyororo kama sufu, manyoya na nyuzinyuzi juu ya uoto mfupi au kati ya mawe. Jike huyataga mayai 3-5.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]