Kendall Ellis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kendall Ellis

Kendall Ellis (amezaliwa Machi 8, 1996) ni mwanariadha wa Marekani[1] Ellis alishinda medali ya dhahabu katika mita 4x400 za kujirudia na shaba katika mchanganyiko wa mita 4x400 kwenye michezo ya olimpiki mjini Tokyo. Alishindana mita 400 kwenye michuano ya dunia ya mwaka 2017 na mwaka 2019,akashinda medali za dhahabu kama sehemu ya awali ya mita  4x400 za kujirudia. Kama kijana,Ellis alichukuwa medali ya dhahabu katika mita 4x400 za kujirudia na shaba katika mita 400 kwenye 2015 Pan American Junior Championships.[2]

Juni 10 mwaka 2018 utofauti wake ulienea kutoka nyuma ya ushindi wake katika mita 1600 za kujirudia kwenye chahe cha University of Southern California tukio la timu na nafasi ya pili kitaifa katika riadha kwenye historia ya programu.[3] Ellis ni bingwa mara 3 kwenye michuano ya NCAA, mara 14 kwenye  NCAA Division I All-American, mara 7 kwenye  Pac-12 Conference, na bingwa mara 5 kwenye Mountain Pacific Sports Federation.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Ellis alishinda medali ya dhahabu kwenye mbio za kujirudia za mita 4x400 na shaba kwenye mchanganyiko wa mita 4x400(akishiriki michezo ya awali) katika michezo ya olimpiki Tokyo

Alikuwa wanne katika mita 400 katika majaribio ya olimpiki mwaka 2020 kwa muda wa sekunde 50.10.

Ellis alishindana katika mita 400 za wanawake na akashinda dhahabu katika mita 4x400 za kujirudia(akishiriki michezo ya awali) katika michuano ya dunia ya riadha mwaka 2020 Januari 2019 alitangazwa kusaini New Balance na baadae akashinda taaluma yake ya kwanza kwenye week hiyo katika  New Balance Indoor Grand Prix.

Ellis alishindana kwenye mita 400 za wanawake na akashinda dhahabu kwenye michuano ya riadha duniani 2017-mita 4x400 za kujirudia upande wa wanawake (akishiriki michezo ya awali) kwenye michuano ya riadha ya duniani 2017.Ellis alishindana kwenye michuano ya riadha ya vijana pan America 2015 na akashinda dhahabu kwenye mita 4x400 za kujirudia na shaba kwenye mita 400.

Ellis ni bingwa wa mwaka wa riadha wa Marekani chini ya miaka 20 mwaka 2015.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "IAAF 2017 Medal Table". Africa Research Bulletin: Political, Social and Cultural Series 54 (8): 21560C–21560C. 2017-09. ISSN 0001-9844. doi:10.1111/j.1467-825x.2017.07859.x.  Check date values in: |date= (help)
  2. Przednowek, Krzysztof; Iskra, Janusz; H. Przednowek, Karolina (2014). "Predictive Modeling in 400-Metres Hurdles Races". Proceedings of the 2nd International Congress on Sports Sciences Research and Technology Support (SCITEPRESS - Science and and Technology Publications). doi:10.5220/0005082201370144. 
  3. Sommerville, Diane Miller (2018-10-01), "Somethin’ Went Hard agin Her Mind", Aberration of Mind (University of North Carolina Press): 120–148, iliwekwa mnamo 2021-10-03 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kendall Ellis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.