Nenda kwa yaliyomo

Kastori wa Apt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Kastori alivyochorwa akikomboa wafungwa.

Kastori wa Apt (pia: Castorius, Castor, Castré; Nimes, baada ya 350 - Apt, 423) alikuwa askofu wa Apt, Vaucluse (leo nchini Ufaransa)[1] tangu mwaka 410 hadi kifo chake.

Kabla yake alikuwa mwanasheria akaoa (395), lakini alikuja kukubaliana na mke wake waende kuishi kama wamonaki. Mwenyewe alianzisha monasteri huko Provence[2].

Kwa ajili ya malezi ya wafuasi wake alimuomba Yohane Kasiano aandike kitabu kipya juu ya mababu wa jangwani [3] .

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Septemba[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • (Kifaransa) Manuscrit de Raymond de Bot, évêque d'Apt (1275-1303), Vie de saint Castor, évêque d'Apt, traduite d'un manuscrit latin du VIII siècle, disparu en 1793 des Archives capitulaires, copie à la Bibliothèque Inguimbertine de Carpentras sous le titre Acta ad firmandam eccl. gall. historiam.
  • (Kifaransa) J. F. de Rémerville de Saint-Quentin, La vie de saint Castor, Apt, 1688.
  • (Kifaransa) G. Barruol, Provence Romane II, Éd. Zodiaque, La Pierre-qui-Vire, 1981.
  • (Kifaransa) G. Semonsu, Castor à Ménerbes, Bulletin de l'Association d'Histoire et d'Archéologie du Pays d'Apt, n° 9, 1985.
  • (Kifaransa) PA Février, San Castore, Évêque d'Apt, et son culte, Provenza Historique, fasc. 146, 1986.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.