Kasoko ya dharuba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kutokea kwa kasoko ya dharuba
Kutokea kwa kasoko kutokana na dharuba (filamu ya maabara ya NASA)

Kasoko ya dharuba (kwa Kiingereza impact crater) ni tundu kwenye ardhi linalotokana na mshtuko wa kugongwa na gimba. Kasoko ina umbo la duara; katikati ni kama shimo na ukingo wake unainuka juu ya uwiano wa mazingira yake. Duniani kasoko zinapatikana mara nyingi kutokana na milipuko ya volkeno au milipuko mingine.

Katika magimba ya angani yenye uso thabiti kuna kasoko nyingi kama matokeo ya kugongwa na magimba kutoka anga la nje. Kwa mfano, kwenye Mwezi wa Dunia kuna kasoko nyingi zilizosababishwa na migongano ya asteroidi au vimondo. Pigo la kitu kigumu linarusha mata iliyopo mahali pa mgongano ikipangwa pembeni kwa tundu hili kwa umbo la ukingo wa mviringo.

Duniani kasoko nyingi kutokana na mishtuko ya aina hii zinasawazishwa baada ya muda fulani kutokana na mmomonyoko wa mvua na upepo; kwenye magimba pasipo angahewa kama Mwezini zinabaki kwa miaka milioni kadhaa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kasoko ya dharuba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.