Kambi za wachawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kambi za Wachawi ni makazi ambapo wanawake nchini Ghana ambao wamekuwa wakishutumiwa kuwa wachawi wanaweza kukimbilia kwa ajili ya kupata usalama. Wanawake katika kambi kama hizo wameshutumiwa kwa uchawi kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa akili. Baadhi ya kambi zinadhaniwa kuwa ziliundwa mwanzoni mwa karne ya 20. Serikali ya Ghana imeanza kuchukua hatua za kuondoa kambi hizo.[1][2]

Kambi za wachawi

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Wanawake wanaoshukiwa kuwa wachawi wakati mwingine hukimbilia kwenye makazi ya wachawi kwa usalama wao mara nyingine ili kuepuka kuuawa na majirani zao.[3][4][5][6][7][2]

Wanawake wengi katika kambi hizo ni wajane na wanashutumiwa na ndugu zao kwani wanaaminika kuwa wanaua waume zao kwa uchawi ili kukamata mali za marehemu.[7] Wanawake wengi waliopo katika kambi za wachawi wanaugua ugonjwa wa akili, jambo ambalo halieleweki vizuri nchini Ghana.[2][5] Katika kambi moja huko Gambaga upande wa kaskazini wanawake hupewa ulinzi na chifu wa eneo hilo na wao humlipa kwa kufanya kazi katika mashamba yake.[6][7]Muungano wa Kampeni ya Kupambana na Madai ya Uchawi-Ghana (AWACC-Ghana) umeripoti kwamba idadi ya watu waliotengwa wanaoishi katika kambi za wachawi inaongezeka na kwamba ugavi wa chakula huko hautoshi.[8][9]

Maeneo[hariri | hariri chanzo]

Kuna jumla ya kambi sita za wachawi nchini Ghana ambazo zina fahamika, zenye jumla ya takriban wanawake wapatao 1,000.[2] Kambi hizo ziko Bonyasi, Gambaga, Gnani, Kpatinga, Kukuo na Naabuli zote ziko Kaskazini mwa Ghana.[10]Baadhi ya kambi hizo zinadhaniwa kuwa ziliundwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.[11][12][13][14][15][16]Serikali ya Ghana imetangaza nia yake ya kufunga kambi hizo na kuelimisha umma kwamba hakuna uchawi.[17][18] Mnamo Desemba mwaka 2014 Waziri wa Jinsia na Ulinzi wa Kijamii Nana Oye Lithur alivunja kambi ya Bonyasi iliyoko katika Wilaya ya Gonja ya Kati na kuwaunganisha tena wakazi wake katika familia zao.[18] Ilipofika mwaka 2015 tayari serikali ya Ghana ilikuwa imefanikiwa kufunga kambi nyingi za wachawi nchini humo.[19]

Soma pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. https://www.actionaid.org.uk/sites/default/files/publications/condemned_without_trial_women_and_witchcraft_in_ghana_report_september_2012.pdf
 2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Ghana witch camps: Widows' lives in exile", BBC News (kwa en-GB), 2012-09-01, iliwekwa mnamo 2022-04-06 
 3. Briggs, Philip; Connolly, Sean (2016-12-16). Ghana (kwa Kiingereza). Bradt Travel Guides. ISBN 978-1-78477-034-1. 
 4. "Archives". Los Angeles Times (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 5. 5.0 5.1 http://www.dw.com/en/ghana-witchcraft-accusations-put-lives-at-risk/a-35988061
 6. 6.0 6.1 Laura Miller (2010-10-25). ""Spellbound": Inside the witch camps of West Africa". Salon (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 7. 7.0 7.1 7.2 Laura Miller (2010-10-25). ""Spellbound": Inside the witch camps of West Africa". Salon (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 8. "Utne". Utne (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 9. "Gov’t disbands Bonyase witch camps". Citi 97.3 FM - Relevant Radio. Always (kwa en-US). 2014-12-16. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
 10. "Bonyase witches’ camp shuts down on Dec. 15". Citi 97.3 FM - Relevant Radio. Always (kwa en-US). 2014-12-08. Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 11. https://www.bbc.com/news/magazine-19437130
 12. "Bonyase witches’ camp shuts down on Dec. 15". Citi 97.3 FM - Relevant Radio. Always (kwa en-US). 2014-12-08. Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 13. "Why are 'witches' still being burned alive in Ghana? | Cameron Duodu". the Guardian (kwa Kiingereza). 2010-12-31. Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 14. http://www.whrin.org/wp-content/uploads/2013/04/Witch-Camp-Report-2011.pdf
 15. https://www.actionaid.org.uk/sites/default/files/doc_lib/ghana_report_single_pages.pdf
 16. https://ec.europa.eu/europeaid/sites/devco/files/article-lucyadams_en.pdf
 17. "Ghana's witch camps: last refuge of the powerless and the persecuted". The Independent (kwa Kiingereza). 2012-08-25. Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 
 18. 18.0 18.1 "Ghana witch camps: Widows' lives in exile", BBC News (kwa en-GB), 2012-09-01, iliwekwa mnamo 2022-04-06 
 19. "Witchcraft accusation". Graphic Online (kwa en-gb). Iliwekwa mnamo 2022-04-06. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kambi za wachawi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.