Kale ya Washairi wa Pemba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kale ya Washairi wa Pemba ni kitabu kilichokusanya mashairi ya kale ya Wazanzibari yaliyoandikwa na washairi wawili walioishi mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni mwa karne ya 19.

Washairi hao wanajulikana kama Kamange na Sarahani na mashairi yao kukusanywa na Abdulrahman Saggaf Alawy [1] na kuhaririwa na Abdilatif Abdalla [2] mshairi wa mashairi ya Sauti ya dhiki [3] na kisha kuchapishwa na Mkuki na Nyota mwaka 2011.

Kitabu hicho kimeelezea hali ya utawala ilikuwepo katika karne hizo mbili katika visiwa vya Pemba na Zanzibar; pamoja na kuelezea siasa kimeelezea pia namna washairi walivyoishi katika karne ya 19 na mwanzo wa karne ya 20.

Kitabu kimeelezea pia namna mashairi mengi yalivyopotea kwa kuchomwa moto wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar na kusababisha kumbukumbu nyingi za tungo hizo za kale kupotea. [4]

Katika kuyaelezea maisha ya kiutunzi kwa washairi kitabu hicho kimeelezea namna washairi hao wawili walivyoweza kuishi kwa kuandikiana mashairi mara kwa mara hadi watu kuhisi kulikuwa na ugomvi baina ya Kamange na Sarahani. Pia kitabu kimeonyesha matumizi ya lugha na ufundi wa kutunga ambao kila mshairi anapaswa kuwa nao.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kale ya Washairi wa Pemba". Mkuki na Nyota Publishers (kwa en-US). 2015-10-21. Iliwekwa mnamo 2020-02-12. 
  2. "Mwandishi aliyeonja mateso ya kalamu", BBC News Swahili (kwa Kiswahili), 2017-01-24, iliwekwa mnamo 2020-02-12 
  3. Maitaria, Joseph Nyehita; Wafula, Richard Makhanu (2019-03-13). "Ushairi wa Abdilatif Abdalla katika Kubainisha Utamaduni wa Waswahili". Journal of Linguistics and Language in Education (kwa Kiingereza) 12 (2): 74–98. ISSN 0856-9965 Check |issn= value (help). 
  4. Kale ya washairi wa Pemba : Kamange na Sarahani. Abdalla, Abdilatif, 1946-, El-Maawy, A. A. A. (Ali A. A.), Alawy, Abdurrahman Saggaf., Sarahani bin Matwar, 1841-1926., Jahadhmiy, Ali bin Said bin Rashid, 1830-1910. Dar-es-Salaam: Mkuki na Nyota. 2011. ISBN 978-9987-08-160-8. OCLC 868218814. 
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kale ya Washairi wa Pemba kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.