Nenda kwa yaliyomo

Juche

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mnara wa Juche mjini Pyonyang, Korea Kaskazini
Raia wa Korea Kaskazini jinsi wanavyojinama mbele ya sanamu za Kim Il Jong na mwanawe Kim Jong Il

Juche ni itikadi rasmi ya Korea Kaskazini. Huelezwa kama "mchango wa kiasili, mtukufu na wa kimapinduzi kwa fikra za kitaifa na za kimataifa" za Kim Il-sung, kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo tangu Vita Kuu ya Pili.

Inasisitiza kwamba "mwanadamu ndiye mtawala wa hatima yake", kwamba raia wanapaswa kutenda kama "mabwana wa mapinduzi na ujenzi wa taifa", na kwamba kwa kujitegemea na kuwa na nguvu, taifa linaweza kufikia ujamaa wa kweli . [1]

Kim Il-sung alianzisha itikadi hiyo ambayo mwanzoni ilitazamwa kama aina ya Umaksi-Ulenin hadi ilipotangazwa kuwa itikadi tofauti na mwanawe na mrithi wake, Kim Jong-il. Kwa hiyo, serikali ya Korea Kaskazini ilifafanua Juche kuwa idadi ya kanuni zinazotumiwa kuhalalisha maamuzi yake ya kisera: kujitegemea kisiasa (자주), kujitosheleza kiuchumi (자립), na kujitegemea kijeshi (자위).

Itikadi ya Kiongozi Mkuu

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Kim Jong-il kuonekana kama mrithi wa Kim katika miaka ya 1970, uaminifu kwa Kiongozi Mkuu ulizidi kusisitizwa kama sehemu muhimu ya Juche.

Mafundisho hayo yanamweleza Kiongozi Mkuu kuwa kiongozi kamili. Tabaka la wafanyakazi si la kujifikiria, bali la kufikiri kupitia kwa Kiongozi Mkuu. Ndiye "ubongo wa juu" (yaani "bwana akili") wa tabaka la wafanyakazi, kwa maana yeye ndiye mwakilishi halali wa tabaka la wafanyakazi. Katika maendeleo ya kihistoria, Kiongozi Mkuu ndiye kiongozi mkuu wa tabaka la wafanyakazi.

Kiongozi Mkuu hutazamwa pia kuwa binadamu asiye na dosari na asiyeweza kuharibika, ambaye hafanyi makosa, daima ni mkarimu na daima anatawala kwa ajili ya watu wengi.

Ukosoaji

[hariri | hariri chanzo]

Juche imefafanuliwa na wakosoaji kama itikadi ya uzalendo mkali [2] inayoachana na mafundisho ya Umaksi-Ulenin. Shin Gi-wook aliandika kwamba "hakuna dalili ya Umaksi-Ulenin au dhana ya Stalin ya utaifa [katika Korea Kaskazini]. Badala yake, serikali inasisitiza umuhimu wa damu ya watu wa Korea, nafsi na sifa za kitaifa".[3]

Brian Reynolds Myers aliona kuwa Juche ina uhusiano zaidi na ufashisti wa Kijapani kuliko Umaksi-Ulenin. [4]

Wachambuzi kadhaa kutoka nchi za magharibi, kama vile Robert E. Kelly, wanaona kuwa Juche ipo tu ili kulinda utawala wa familia ya Kim juu ya siasa nchini Korea Kaskazini. [5]

  1. Juche Idea: Answers to Hundred Questions. Pyongyang: Foreign Languages Publishing House. 2014.
  2. Fisher, Max (6 Januari 2016). "The single most important fact for understanding North Korea". Vox. Iliwekwa mnamo 10 Aprili 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Shin, Gi-wook (2006). Ethnic Nationalism in Korea: Genealogy, Politics, and Legacy. Stanford University Press. ISBN 9780804754088.
  4. "If North Korea isn't communist, then what is it?". www.lowyinstitute.org (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-07. Iliwekwa mnamo 2021-12-07.
  5. "If North Korea isn't communist, then what is it?". www.lowyinstitute.org (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-07. Iliwekwa mnamo 2021-12-07."If North Korea isn't communist, then what is it?" Ilihifadhiwa 7 Desemba 2021 kwenye Wayback Machine.. www.lowyinstitute.org. Retrieved 7 December 2021.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]