Nenda kwa yaliyomo

Jorge Carlos Fonseca

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jorge Carlos de Almeida Fonseca (amezaliwa 20 Oktoba 1950) ni mwanasiasa wa Cape Verde, mwanasheria na profesa wa vyuo vikuu ambaye amekuwa Rais wa Cape Verde tangu mwaka 2011.

Awali alihudumu kama Waziri wa Mambo ya nje kutoka mwaka 1991 hadi 1993. Aliungwa mkono na Movement for Democracy (MpD), alishinda uchaguzi wa rais wa 2011 katika raundi ya pili ya kupiga kura.

Uchaguzi wa Urais ulipofanyika Cape Verde mnamo 2 Oktoba 2016, alichaguliwa tena kwa asilimia 74.08 ya kura.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jorge Carlos Fonseca kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.