Jeremias Nguenha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jeremias Nguenha (19 Machi 1972, Inhambane - 3 Mei 2007, Maputo) alikuwa mwanamuziki wa nchini Msumbiji.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Nguenha alianza kuimba katika kanisa la 'Assembleia de Deus' na wakati huo alikua kama mchungaji.

Alianza kuimba ili kueneza ujumbe wa ukosefu wa haki za kijamii na ujumbe wa kuelimisha watu. Mnamo mwaka 1994 na 1995 nyimbo zake zilionekana kama uchawi kutokea mwanzoni kabisa kwenye redio, kwa kuwa wimbo wake mashuhuri kabisa ni 'Vadhla Vôche' maneno yake katika wimbo yalikuwa ni: 'kemea ubinafsi, unafiki na ufisadi ambavyo vimeichafua jamii'. Mtindo wake pia ulikuwa unawashtua watu wa Msumbiji na alijionyesha akiwa na mavazi ya kijeshi na mtindo wa kunyoa nywele kama wanajeshi, na mara nyingi alikuwa na biblia jukwaani. Muda mfupi baadae alitoa kibao chake kikubwa kabisa cha La Famba bicha ("The line goes on").

Mwaka 2001, alipokea tuzo ya Taifa nchini Msumbiji ( Ngoma Msumbiji) kwa ajili ya wimbo wake maarufu zaidi. Katika mwaka huo huo, rais wa wakati huo - Joaquim Chissano - anamkaribisha kwenye makazi rasmi ya Palácio da Ponta Vermelha.

Alikuwa pia mchezaji wa mpira wa miguu lakini alicheza katika nchi ya Swaziland na Afrika Kusini. Hata hivyo alipata jeraha la goti ambalo lilifanya kazi yake imalizike. Nguenha pia alifanya kazi kama mwigizaji.[1] [2]

Mnamo 3 Mei 2007, akiwa na umri wa miaka 35, taarifa ya kifo chake kutokana na ugonjwa ilitikisa nchi nzima ya Msumbiji na chama cha muziki. Chama cha muziki punde kinataka wasanii wa Msumbiji wawe na hali nzuri kwa wasanii kwani wengi wao walikufa kwa ugonjwa, bila kuwa na hali za fedha za kumudu matibabu bora ya afya kwa hali zao. Katika miaka iliyopita, shirika la muziki lilikuwa likishughulika na hasara mfululizo kwa wasanii kutokana na ugonjwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Morreu Jeremias Nguenha, um dos músicos mais críticos do poder". Noticias Lusofonas (kwa Kireno). 4 May 2007.  Check date values in: |date= (help)
  2. "Faleceu esta noite o músico jovem moçambicano Jeremias Nguenha". Moçambique para todos (kwa Kireno). 4 May 2007.  Check date values in: |date= (help)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jeremias Nguenha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.