Jabuha Asadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Gamma Leonis (γ Leo), also named Algieba Jabuha Asadi


Jabuha Asadi
(Gamma Leonis, Algieba)
Asadi Leo.png
Kundinyota Asadi (pia: Simba, Leo)
Mwangaza unaonekana 2.08 [1]
Kundi la spektra A: K0 III B: G7 III
Paralaksi (mas) 25.07 ± 0.52
Umbali (miaka ya nuru) 130
Mwangaza halisi A: –0.27 B: +0.98
Masi M☉ A: 1.23
Nusukipenyo R☉ A: 31.88 B: 10
Mng’aro L☉ A: 320 B: 40
Jotoridi usoni wa nyota (K) A: 4470 B: 4980
Majina mbadala γ Leonis, 41 Leo, BD +20°2467, GCTP 2423.00, HIP 50583, NSV 4823, LTT 12764/12765, WDS 10200+1950


Jabuha Asadi (ar., lat. & ing. Algieba pia γ Gamma Leonis [2], kifupi Gamma Leo, γ Leo) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota ya Asadi (pia: Simba) (Leo). Jabuha Asadi ni nyota maradufu iliyotambuliwa kuwa na angalau sayari moja.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jabuha Asadi inayomaanisha “Paji la Simba” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [3]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema kwa kawaida الأسد جبهة jabha al-asad inayomaanisha „paji la simba ". Jina hili lilmejadiliwa mara nyingi kwa sababu katika picha zote za kundinyota hii si sehemu ya kichwa zaidi la nywele za shingoni lakini unajimu wa Waarabu unajua «  manzili za mwezi » na mojawapo ni « al jabha » inayojumlisha nyota kadhaa za Asadi (Simba) kwa hiyo inawezekana jina lilitokea hapa [4]. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota ya γ1 kwa jina la "Algieba" [5] . Hivyo sehemu nyingine ya nyota pacha γ2 haina jina.

Gamma Leonis ni jina la Bayer ingawa Gamma ni herufi ya tatu katika Alfabeti ya Kigiriki na Jabuha Asadi ni nyota angavu ya pili katika Asadi (pia: Simba) - Leo.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Jabuha Asadi inatambuliwa kuwa nyota pacha kwa kutumia darubini ndogo.

Nyota kuu ina mwangaza unaoonekaka wa +2.28 ikiwa katika kundi la spektra K1-III. Jotoridi usoni ni K 4,470 na mng’aro wake kwenye Lo 180. Nyota ya B huwa na mwagaza unaoonekana wa mag +3.51 iko katika kundi la G7 III. Zinazungukana kwa umbali wa vizio astronomia 170 katika muda wa miaka 500 au zaidi. Zote mbili zimeshakwisha kuyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu zikapanuka katika hatua iliyofuata.

Mwaka 2009 watafiti wa Korea, Ukraina na Ujerumani walitambua mabadiliko katika nuru ya spektra zilizoonyesha uwezekano wa kuwepo kwa sayari yenye masi 8-9 za Mshtarii (Jupiter) inayozunguka Jabuha Asadi A katika muda wa siku 429. [6].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. vipimo kufuatana na Han & alii (2009)
  2. Leonis ni uhusika milikishi (en:genitive) wa "Leo" katika lugha ya Kilatini na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa, Beta, Gamma Leonis, nk.
  3. ling. Knappert 1993
  4. Allen (1899). uk. 259
  5. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  6. Han & alii (2009)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Han, Inwoo; Lee, B. C.; Kim, K. M.; Mkrtichian, D. E.; Hatzes, A. P.; Valyavin, G. (2010). "Detection of a Planetary Companion around the giant star γ-1 Leonis". Astronomy and Astrophysics. 509: A24. [1]