Irene Birungi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Irene Birungi Mugisha
Nchi Uganda
Kazi yake Mjasiriamali, mwandishi wa habari
Cheo mchambuzi wa habari
Ndoa ameolewa
Watoto watatu


Irene Birungi Mugisha (née Irene Birungi) ni mjasiriamali, mwandishi wa habari toka nchini Uganda na hufanya kazi kama katibu binafsi katika ofisi za utawala wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, kuanzia Septemba mwaka 2017.[1]

Pia Mugisha ni muasisi wa All Round Consult, uhusiano wa kimataifa na taasisi ya habari iliyopo jijini Kampala, mji mkuu wa Uganda. Mnamo mwezi Oktoba mwaka 2010, aliweza kuwa meneja wa kwanza wa kike mwandishi wa habari nchini Uganda baada ya kupata uteuzi katika shirika la habari la Uganda lijunikalo kama Shirika la habari la Taifa la Uganda ([[Uganda Broadcasting Corporation). Mnamo mwaka 2013, alikuwa mhariri mkuu na kuwa mzalisha vipindi katika televisheni na CNBC Africa. Alikuwa pia mwandishi wa gazeti la Daily Monitor[2] na New Vision kuhusiana na masuala ya uchumi.[3]

Kazi ya Uandishi wa Habari[hariri | hariri chanzo]

Mugisha alipata umaarufu katika tasnia ya uandishi wa habari baada ya kuajiriwa kama mchambuzi wa habari katika kituo kijulikanach kama WBS Television, (halifanyi kazi kwa sasa). Baada ya miaka mitano kupita, aliweza jiunga na shirika la habari la taifa lijulikanayo kama (Uganda Broadcasting Corporation) luninga (UBC Television) kama mzalishaji wa vipindi na mhariri wa masuala ya biashara. Mnamo Octoba mwaka 2010, aliweza teuliwa kama meneja wa luninga katika shirika la utangazaji wa taifa lijulikanalo kama (Uganda Broadcasting Corporation), mwanamke wa kwanza nchini Uganda kushika nafasi hiyo katika shirika la Taifa la Utangazaji.[4]

Mnamo mwaka 2013, alijiunga na CNBC Africa na kuwa mhariri kiongozi na mzalisha vipindi katika mashirika yao nchini Uganda na Rwanda, ambapo aliweza kuwa mtangazaji katika maonyesho maarufu "Doing Business in Rwanda.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Mugisha aliolewa na Maurice Mugisha, ambaye ni mkurugenzi msaidizi katika shirika la utangazi la habari la taifa na hufanya kazi kama mshereheshaji katika hafla tofauti tofauti. Hapo awali alifanya kazi kama mkuu wa idaraya ya habari katika kituo cha taifa kijulikanacho kama Nation Media Television Uganda.[5] Mugisha ni mama wa watoto watatu, wakiume kutoka mahusiano wake wa awali na mabinti wawili kwa mke wake wa sasa.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Gee Mukama (21 September 2017). "Maurice Mugisha's Wife Lands A Juicy Job in Statehouse". Kampala: Howwe Entertainment. Iliwekwa mnamo 12 November 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. Irene Birungi Mugisha (5 February 2016). "Uganda's public health sector has undergone fundamental change". Daily Monitor. Kampala. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-17. Iliwekwa mnamo 12 November 2018.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. Irene Birungi Mugisha (16 December 2016). "What lower middle income status means to local Ugandans". New Vision. Kampala. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-17. Iliwekwa mnamo 12 November 2018.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "Awel denies list of spin masters who made Museveni hate PR". The Edge. Kampala: The Edge Uganda. 12 September 2018. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-17. Iliwekwa mnamo 12 November 2018.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. Agencies (12 October 2018). "Revamp: Uganda National Broadcasting Television poaches NTV’s Maurice Mugisha". Kampala: PMLDaily.com. Iliwekwa mnamo 12 November 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. Okuda, Ivan. "I’m older than Maurice, but so what?". Daily Monitor. Iliwekwa mnamo 12 November 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Irene Birungi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.